Pages

Pages

Tuesday, March 6, 2012

LILIAN INTERNET, AKIDA KUTAMBULISHWA KESHO NYUMBANI LOUNGE

ONYESHO maalum la utambulisho wa wasanii wapya waliojiunga na bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa Band, mnenguaji Lilian Tungaraza ‘Internet’ na mpapasa Kinanda Ally Akida linatarajiwa kufanyika KESHO katika ukumbi wa Nyumbani Lounge.
Internet aliyekuwa akifanya kazi katika bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta’ na Akida aliyerkuwa mwanamuziki wa kujitegemea walijunga na MAshujaa wiki iliyopita baada ya kusaini mktaba wa miaka miwili.
Mbali ya Mashujaa , onyesho hilo pia litapambwa na Machozi Band inayomilikiwa na Mwanadada Lady Jay Dee ambapo kutakuwa na mambo mazuri ya kuvutia.
“Si onyesho la kukosa kwa mpenda muziki wa dansi kwani pamoja na utambulisho wa wasanii wetu wapya, bendi hizi zinatarajiwa kukonga kwa nyimbo zake kadhaa sambamba na shoo ya nguvu toka katika sdafu zao za unenguaji,”Alisema Luhanga.
Naye Lilian akizungumzia hatua ya kuhamia kwake Mashujaa alisema kilichompeleka huko ni maslahi mazuri mazuri anayolipwa kwa kazi yake sambamba na fedha ya kujikimu kwa masuala mbalimbali ikiwemo matibabu, usafiri na nyumba.
Alisema pamoja na hilo amekwenda huko kwa ajili ya kupata uzoefu zaidi katika harakati zake hizo za kusaka maisha kupitia muziki huku akiwaahidi mambo makubwa mashabiki wa bendi hiyo na muziki wa dansi kwa ujumla.
Internet amekuwa msanii wa pili kunyakuliwa na Mashujaa Musica hivi karibuni toka Twanga Pepeta ambayo mapema mwaka huu ilimchukua mwimbaji Charles Gabriel ‘Charlz Baba’ kwa lengo la kuimarisha kundi lao.

No comments:

Post a Comment