Pages

Pages

Wednesday, March 28, 2012

SINTA SASA ASAKA DUME LA KUMZALISHA


     STAA wa Filamu na Maigizo Bongo, ambaye kwasasa anachapa mzingo Kwenye kipindi cha Hatua Tatu kinachorushwa hewani kupitia 100.5 Times FM, Sintah Manongi 'Sintah JLO Africa', juzikati alifyatuka kwakusema kuwa anahitaji bwana wa kuzaa naye maana amezidi kusema kila  kona na ndugu na marafiki zake wa karibu.
  Akigonga stori mbili tatu na mwandishi wa habari hizi, Machi 27 mwaka huu Sintah alisema kuwa, amefikia kusema hivyo kwakua tayari umefikia wakati wake wa kuitwa mama maana siku zinazidi kwenda mbele na  akisema asubiri ndoa ndiyo azae bado itazidi kumchukua muda mrefu kumpata atakayeendana naye kitabia kama ndoto zake zilivyo siku zote.
"Niko Sileas na hili na wala sitanii tena maana sasa nimezidi kukoseshwa raha na marafiki zangu kila mmoja ukiongea naye habari zinazohusiana na mtoto basi utasikia ananisema tena wakati huo anakuwa hatanii hata kidogo, sasa kuepusha maneno nitazaa pale tu nitakapopata mwanaume wa kuzaa naye, alisema Sintah a.k.a JLO Africa

No comments:

Post a Comment