Pages

Pages

Monday, June 4, 2012

AKUOT PHILIP SUZAN NDIYE MISS EAST AFRICA SOUTHERN SUDAN



Mrembo atakayeiwakilisha Nchi ya Sothern Sudan katika mashindano ya Miss East Africa 2012 amepatikana.
Mrembo huyo  ni  Miss Akuot Philip Suzan (20)  mwenye urefu wa futi 6.1 anaekaa Juba, Sudan  ni mwanamitindo Nchini humo na anatarajia kujiunga na chuo kikuu cha makelele Nchini Uganda mwaka huu.
Warembo ambao tayari wameshapatikana kutoka katika Nchi mbalimbali kwa ajili ya mashindano hayo ni mwakilishi wa Eritrea: Miss Rahwa Afeworki (22), kutoka Ethiopia ni: Miss Lula Teklehaimanot (19) na Miss Ayisha Nagudi (23) ambae ni mwakilishi wa Uganda.
Nchi zilizobaki zinaendelea kutafuta wawakilishi watakaoziwakilisha Nchi zao katika mashindano ya Miss East Africa 2012 ambayo yatazishirikisha Nchi 16 za ukanda huu ambazo ni Tanzania (wenyeji), Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi. Nchi zingine ni Southern Sudan, Somalia, Djibouti, Eritrea, Ethiopia pamoja na visiwa vya Mauritius, Madagascar, Comoros, Reunion na Seychelles.
Mashindano ya Miss East Africa ndio mashindano makubwa ya urembo kwa ukanda huu wa Africa.
Fainali za mashindano ya Miss East Africa ambazo huandaliwa na kumilikiwa na Kampuni ya Rena Events Ltd, zitafanjika tarehe 07 mwezi September mwaka huu jijini Dar es salaam, Tanzania.

No comments:

Post a Comment