Pages

Pages

Monday, June 4, 2012

MPOKI,NGWASUMA KUPAMBA MISS KIGAMBONI 2012

Bendi  dansi yaFM maarufu kama wazee WANGWASUMA  pamojana msanii wa vichekesho MPOKI watatoa burudani ya anina yake katika shindano lakumsaka malkia wa kitongoji cha  Kigamboni City 2012' litakalofanyika Juni15   mwaka huu katika  ukumbi wa Navy Beach ulioko huko Kigambonihapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana jijini, Mratibu wa shindano hilo,Somoe Ng'itu, bendi ya FM inafahamika kwa kutoa burudani nzuri kwa mashabiki wamuziki wa dansi nchini .

Kuhusiana na msanii MPOKI, SOMOE amesema kuwamchekeshaji huyo ambaye pia ni mkazi wa KIGAMBONI amekuwa ni kati yawaburudishaji katika sanaa ya uchekeshaji na kupendwa na watu wa rika zotehivyo mashabiki wa urembo wataweza kupata burudani ya uhakika .

Mratibu huyo kutoka kampuni ya K& L, alisemakuwa  Jumla ya warembo 15 wanaendeleakujifua katika kambi ya mazoezi chini ya mwalimu wao miss TEMEKE HAWA ISMAILambaye anashirikiana na mshiriki wa miss TANZANIA mwaka jana BLESSING NGOWI.

Amewataja warembo hao kuwa ni pamoja na CAROLYNEDANDU,FATINA FRANSIS,EDDA SLYVESTER,AISHA MUSSA,ROSEMARY PETER,DOREENKWEKA,CAROLINE PETER,AGNES GOODLUCK,SOPHIA MARTINE,ROSEMARY DEOGRATIUS,BEATRICEBONIFACE,JULIETH PHILIP na KHADIJA KOMBO.

"Kigamboni ni zaidi ya kitongoji, tunaamini shindano letu litakuwa namvuto na hadhi ya kipekee kama eneo lake lilivyo," aliongeza.

Alisema kuwa warembo watakaofanya vizuri watapata nafasi ya kuwakilishakitongoji hicho katika mashindano ya kanda ambayo yatafanyika baadaye mwakahuu.
 
Aliwataja wadhamini ambao tayari wamethibitisha kudhamini shindano hilo nipamoja na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Redd's,Dodoma Wine na NSSF,Hope country Motel,Norbro’s Collections,Screenmasters,Global Publishers.

Salha Israel kutoka Kanda ya Ilala ndiye mremboanayeshikilia taji la taifa ambapo mwaka huu ratiba ya mashindano hayoimebadilika.

No comments:

Post a Comment