Pages

Pages

Tuesday, July 17, 2012

IRENE BWIRE AWA MISS UTALII KAGERA 2012

 Miss Utalii Kagera 2012 Miss Irene Bwire (katikati) na mshindi wa pili Miss Jania Abdul (kushoto)  na Miss Mayor Kashumba mshindi wa tatu (kulia)
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Mh Mama Pangani akifungua Onyesho hili rasmi
Mrembo Irene bwire ameibuka mshindi wa Taji la Miss Utalii Kagera 2012, katika shindano lililofanyika katika ukumbi wa Linas Club mjini Bukoba mkoani Kagera siku ya jumamosi tarehe 14-7-2012. 
Irene alitwaa taji hilo kwa kuwashinda warembo wengine 14, katika shindano ambalo mkuu wa Wilaya ya Bukoba mama Pangani alikuwa mgeni rasmi. Mrembo Jania Abdul alikuwa mshindi wa pili na Mayor Kashumba alikuwa mshindi wa tatu, hivyo wote pamoja na mshindi wa nne,watano na mshindi wa taji la Miss Utalii Vipaji watawakilisha mkoa wa kagera katika fainali za Miss Utalii Tanzania 2012- Kanda ya Magharibi,zitakazofanyika mkoani Mara, mwezi Oktoba 2012.

Katika shindano hilo ambalo lilisindikizwa na burudani za muziki wa asili na wa kizazi kipya wakiwemo bendi ya Diamond Sound, msanii BK Sunday  na makundi ya ngoma za asili za mkoa wa kagera,shindano hilo
liliandaliwa na Dinner Fashion,huku Miss Utalii Kilimanjaro 2012 Evamary Gamba akiwa ni mwalimu wa warembo.
Mgeni rasmi aliwapongeza waandaaji kwa kufanikiwa kuandaa shindano hilo ambalo kwa kiasi kikubwa limekuwa ni kichocheo cha kutangaza utalii na utamaduni wa mkoa wa kagera. 
Aidha 
alisema kuwa serikali na mkoa wa Kagera wanathanini sana mchango wa shindano hilo katika kuhamasisha na kutangaza utalii na utamaduni wa Tanzania pia mianya ya uwekezaji, na kuwataka wadau mbalimbali
kuliunga mkono kwa kudhamini shindano hilo kla linapofanyika

No comments:

Post a Comment