Pages

Pages

Tuesday, July 17, 2012

MISS UTALII KINONDONI YASOGEZWA MBELE KUPISHA MWEZI MTUKUFU

  Shindano la kumsaka myange wa Utalii wilaya ya Kinondoni 2012 limesogezwa mbele kutokana na kuanguangukia mwanzoni mwa mfungo wa ramadhani ambapo kamati husika imetoa tamko la kusogeza mbele shindano hilo kupisha mfungo mtukufu wa ramadhani ambao unaanza mwishoni mwa wiki hii.
  Chanzo cha habari kinasema kuwa sababu kuu ya kuhamisha tarehe husika ya shindano toka tarehe 20 julai mpaka iddi pili mwezi wa nane ni kuondoa taswira tofauti ambapo baadhi ya washiriki na wanakamati kuwa waumini wa dini ya kiislamu hivyo kamati ikaona vyema kupeleka mbele shindano hilo ambapo limekua gumzo jijini Dar es salaam.
  Taarifa kamili kuhusu tarehe shindano hilo itatangazwa rasmi kupitia vyombo vya habari hivi punde,tunaomba radhi kwa usumbufu ila tumefanya hivyo kueshimu taratibu za kidini hususani kipindi hiki cha mwezi mtuku wa ramadhani.

No comments:

Post a Comment