Pages

Pages

Thursday, August 2, 2012

MISS MWANZA 2012/13 KUFANYIKA AGOSTI 31

Mrembo wa mkoa wa Mwanza 2012/13 atapatikana ijumaa ya agosti 31 katika viwanja vya Yatch Club Mwanza.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na muaandaji wa kampuni ya Sisi Entertainment John Doto, amesema shindano hilo linalovuta hisia za wengi ndani ya mkoa wa Mwanza na kanda ya ziwa kwa ujumla, litashirikisha warembo tariban 20 kutoka wilaya zote za mkoa Mwanza.
John Doto amesema warembo wote watakaa kambini kwa wiki mbili, ambapo kambi rasmi itaanza tarehe 20 agosti mwaka huu katika hoteli ya Isamilo Lodge. Shindano la Redds Miss Mwanza 2012/13, lilisogezwa mbele kufuatia mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Wakiwa kambini warembo watapata fursa ya kujifunza Mitembeo, Tabasamu, ufahamu wa kujieleza pamoja na kuvumbua vipaji mbalimbali.
John Dotto pia amesema warembo watakua na ziara ya kwenda kwenye mbuga za wanyama Serengeti, kutoa misaada kwa watoto yatima, vikongwe pamoja na kufanya usafi kwenye moja
ya Hospitali Jijini Mwanza na moja ya barabara za Mwanza.
Kwa miaka ya hivi karibuni, Mkoa wa Mwanza umekua ukitoa warembo wanaofanya vizuri mashindano ya Taifa.
Itakumbukwa Mwaka 2008 Nasreem Karim na Mwaka 2009 Miriam Gerald waliweza kushika Mataji ya Miss Tanzania wakitokea mkoa Mwanza.

No comments:

Post a Comment