Pages

Pages

Wednesday, September 12, 2012

MISS TEMEKE 2012 YAZINDUKA

    Wanyange  15 wa Redd's Miss Temeke, ambao wameanza rasmi kambi yao katika Club ya TCC Chang'ombe tayari wa kinyang'anyiro cha kanda hiyo, jana safu ya wakufunzi imeongezewa nguvu baada ya Top Model, Leyla Bhanji naye kuanza kuwafunda.

Warembo hao ambao wameanza programu ya shoo kwa wiki iliyopita, chini ya ukufunzi wa Dickson Daud kutoka kikundi cha THT,  ambapo ilikuwa ni wiki ya kujiweka sawa zaidi kwa shoo ya ufunguzi ambayo itakuwa tofauti sana kiuchezaji wake, kuwa imezingatia urembo zaidi na umri wa warembo katika utumiaji wa jukwaa.

Warembo hao wanaotoka katika vitongoji vya Kigamboni, Kurasini na Chang'ombe ambapo kila sehemu wametoka warembo watano ambapo washindi watatu wa kwanza watapata fursa ya moja kwa moja kushiriki Redds Miss Tanzania 2012, Ijumaa iliyopita wote walipata fursa ya kuangalia shoo iliyofana ya Redd's Miss Ilala katika ukumbi wa Nyumbani Lounge.

Warembo hao ni Agness Goodluck, Angela Gasper, Flaviana Maeda,Edna Sylvester, Catherine Masumbigana, Khadija Kombo, Neema Doreen, Flora Kazungu, Lilian Joseph, Elizabeth Peter, Elizabeth Boniphace, Jesca Haule, Zulfa Bundala, Mariam Ntakisivya na Esther Albert.

No comments:

Post a Comment