Pages

Pages

Wednesday, September 12, 2012

BREAKING NEWS: BALOZI WA MAREKANI NCHINI LIBYA AUWAWA


 
Balozi wa Marekani nchini Libya amefariki baada ya kushambuliwa na watu waliokuwa wamejihami na kuvamia ubalozi wa Marekani Mashariki mwa mji wa Benghazi.
Balozi huyo alisemekana kuwa miongoni mwa maafisa wengine wa ubalozi waliouawa kufuatia maandamano kuhusu filamu iliyotolewa nchini humo ikimkejeli Mtume Muhammad.
Maandamano ya kupinga filamu hiyo pia yalifanyika mjini Cairo dhidi ya ubalozi wa Marekani.
Wakati huohuo, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bi. Hilary Clinton, amelaani mashambulizi hayo.
Serikali ya Libya imetaja shambulio hilo kama kitendo cha uoga.
Ubalozi huo uliteketezwa na watu waliojihami kwa bunduki kulalamikia filamu moja iliyotengenezewa nchini Marekani ambayo wanasema inamdhihaki Mtume Mohammed.
Wanamgambo hao wanaoripotiwa kuwa na ufungamano na kundi la waislamu wenye msimamo mkali walitumia maguruneti ya kurushwa kwa roketi kuvamia ubalozi huo kabla ya kuiteketeza. Maafisa wa Libya wameiambia BBC kwamba hali imetulia kwa sasa.
Machafuko hayo ya Libya yalijiri saa kadhaa baada ya maelfu ya waandamanaji kukusanyika nje ya ubalozi wa Marekani mjini Cairo kuelezea hasira zao kuhusu filamu hiyo kumhusu Mtume Mohammed.
Kwa wakati mmoja waandamanaji hao waliingia ndani ya ubalozi huo na kuichana bendera ya Marekani na kurejesha yao.

No comments:

Post a Comment