Pages

Pages

Saturday, September 1, 2012

WAREMBO 5 WAINGIA FAINALI ZA VIPAJI SHINDANO LA REDD's MISS KANDA YA MASHARIKI 2012

 Warembo wa 5, waliofanikiwa kutinga katika hatua ya Fainali ya shindano la Miss Kanda ya Mashariki, baada ya kuchuana vikali katika shindano lao dogo la Redd's Miss Kanda ya Mashariki Talent, lililofanyika jana usiku kwenye Hoteli ya Usambara, mjini Morogoro. Kutoka (kushoto) ni Mrembo, Joyce Baluhi, Shakhila Hassan, Zuhura Gola, Irene Veda na Salvina Kibona, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa washindi.
 Mrembo, Rose Lucas, akionyesha umahiri wake kwa kushambulia jukwaa ipasavyo kujaribu bahati yake kwa kuwakomvis Majaji, wakati wa shindano hilo.
 Mrembo, Shakhila Hassan, akiimba wimbo wa dini, Ebeneza na kuwapagawisha Majaji na mashabiki waliohudhuria onyesho la mpambano huo jana usiku.
 Mrembo, Joyce Baluhi, akisebeneka na wimbo wa Demu Mwigizaji wa Tunda Man, na kuwakosha vilivyo, Majaji na mashabiki waliohudhuria shindano hilo.
 Mrembo, Irene Thomas, akishambulia jukwaa kwa kucheza Dancehall........
 Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa pili kushoto) akiwa meza kuu na Miss Tanzania 2010, Geneviv Emmanuel (kulia) na Miss Morogoro 2010, Asha Saleh, wakifuatilia shindano hilo.
 Baadhi ya wadhamini wa shindano hilo pamoja na mawakala wa Mikoa pia walikuwepo kuwakilisha, (kushoto) ni mmoja kati ya wadhamini wa shindano hilo, Kitwe General Traders.
 Sehemu ya mashabiki waliohudhuria shindano hilo.
 Sehemu ya mashabiki waliohudhuria shindano hilo, 'kuona na kunywa kikali'.....
 Washiriki wakicheza wimbo wao wa ufunguzi wa shoo hiyo kwa pamoja.
 Majaji wakishauliana jambo wakati shindano hilo likiendelea..........
 Hapa ni mshiriki, Irene Veda, akijifua kwa kupuliza Sax phone kabla ya kuanza kwa shindano hilo...
 Hapa ni kabla ya kuanza shindano hilo, warembo wakipiga picha ya pamoja kushoo Love.
 Namba za Bahati zilizotinga Tano Bora ...............
Mrembo, Irene Veda, akiimba na kupuliza Sax Phone......
Jana ilikuwa patashika na nguo kuchanika kwa warembo wa Kanda ya Mashariki katika kinyang'anyiro cha kumtafuta Redds Usambara Safari Lodge Miss Talent 2012.
Warembo kutoka mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na Morogoro walichuana vikali katika kitimtim hicho, huku mrembo kutoka mkoa wa Lindi akiwaacha hoi wahudhuriaji baada ya kupanda jukwaani akipuliza midomo  ya bata maarufu kama Saxphone.
Majaji wa shindano hilo walichagua warembo 5 tu waliofanikiwa kupita katika hatua hiyo. 
na fainali itakuwa hapo kesho [leo] wakati washiriki wote watapanda tena jukwaan kumtafuta mrembo wa Kanda ya Mashariki 2012. pamoja na Balozi wa Usambara Safari Lodge 2012.
Shindano hilo ambalo litafanyika katika hotel ya Nashela, linadhaminiwa na 
Redds,  Dodoma Wine, Usambara Safari Lodge, Sufian Mafoto = Spm, Chilakale Resort,B=Ze Hotel ,Cloud Fm ,Endepa, Jambo Leo,Simple &Amp; Easy Car, Kitwe General Trader.
Shindano la Redds Miss Kanda ya Mashariki linataraji kufanyika kesho Septemba 1, 2012 katika Hoteli ya Nashera Mjini Morogoro. picha zaidi zitawajia hivi punde.

No comments:

Post a Comment