Pages

Pages

Sunday, September 2, 2012

ROSE LUCAS ATWAA TAJI LA REDD'S KANDA YA MASHARIKI 2012

Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2012, Rose Lucas, akipunga mkono baada ya kutangazwa mshindi na kujinyakulia taji hilo kwa kuwashinda warembo wenzake 10 katika shindano hilo lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Hoteli ya Nashera  'mji kasoro Bahari'.
Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2012, Rose Lucas (katikati) akipunga mkono kwa furaha akiwa na washindi wenzake, mashindi wa pili Irine Veda (kulia) na Mshindi wa tatu Joyce Baluhi, baada kutangazwa washindi wa shindano hilo lililofanyika mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo, Warembo hawa wote watashiriki shindano la Redd’s Miss Tanzania 2012 baadae mwaka huu.
 
Washiriki wa Shindano la Urembo la Redd’s Miss Kanda ya Mashariki 2012 waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kutangazwa kuingia katika hatua hiyo. Kutoka kushoto ni 6. Zuhura Gora, 7. Irene Veda, 4. Salvina Kibona, 9. Rose Lucas na 5. Joyce Baluhi.
Warembo wa Redds Miss Kanda ya Mashariki wakicheza show yao ya pamoja ya ufunguzi wa shindano lao lililofanyika Hotel ya Nashera Mjini Morogoro usiku wa kuamkia leo.
Wandaaji wa mashindano ya Mikoa iliyoleta washiriki wa Miss Kanda ya Mashariki wakitambiana huku Mwandaaji wa Mkoa wa Lindi, Ramadhan Shaha (katikati) akionesha ishara ya ushindi aitumiayo mkiambiaji wa Kimataifa wa Jamaika Bolt. Shaha alifanikiwa kutoa mshindi wa pili wa mashindano hayo. Wengine kushoto ni Mwandaaji wa Mtwara, Rajab Mchata, Mwandaaji wa Morogoro, Frank Ezekiel na kulia kabisa ni Mama Mchata

No comments:

Post a Comment