Pages

Pages

Thursday, October 4, 2012

SCORPION GALZ KUNDI LA MUZIKI WA KISASI KWA MAASIMU WAO



WAKATI wimbi kubwa la wasanii wa bongo movie wakikimbilia kufanya muziki huku ndani yake wakipigana vijembe, kundi la Scorpion Galz, linaloundwa na wasanii Jini Kabula, Isabella, na Rashida Wanjara, limedai kuwa kazi kubwa watakayokuwa wanaifanya ni kuwapa makavu yao wale wote waliokuwa wanawazungumzia mbaya kuwa wao wanaishi mjini kwa kutengemea nguvu za wanaume.

Wadada hao wote wametokea kwenye mashindano ya ulimbwende, ambapo awalidai kuwa hakuna kitu kinachoshindani kwani walipanga kuigia kwenye muziki muda mrtefu lakini kila mmoja alikuwa na mambo yake anamalizia.

Kabula alidai kuwa wale wote waliokuwa washinda wakiwasema anaamini sasa ni wakati wao wa kupewa majibu yao kwani walikuwa wakiwavutia kasi na kuongeza kuwa wapo wengine ambao wanaanza kujirudi baada ya kuona wanaanza kufanya vizuri.

“Tunafanya muziki kama kawa kama dawa lakini lazima tuwapa makavu yao wale wote waliokuwa wanatusema vibaya, pia nachoweza kusema ni kwamba tunahitaji kutejka mashabiki kutokana na uwezo wetu ingawa ndo kwanza tunaanza lakini naamini mambo yatakuwa poa tu,” alisema.

Hata hivyo alidai kuwa wanahitaji kupata sapoti kubwa kutoka kwa mashabiki wao ambao walikuwa wanamkubali kwenye filamu na tamthilia, lakini sasa wampe sapoti na kwenye muziki ambao ndiyo kwanza amaenza.

Aliongeza kuwa suala la kuishi kwao mjini kwa kutengemea wanaume hawaoni kama ni ishu kubwa sana kwani wapo wanawake wengi wa bongo movie ambao wanaishi mjini kwa mikono ya wanaume lakini hawasemwi.

No comments:

Post a Comment