Pages

Pages

Sunday, November 11, 2012

BREAKING NEEEEEEEWS....MKURUGENZI MKUU WA BBC AJIUZURU WADHIFA WAKE


Taarifa hiyo kwa makosa ilimshutumu aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati wa serikali ya Conservative , Lord McAlpine, kwamba alihusika katika kashfa ya kudhalili
sha watoto.
Tayari shirika la BBC limekuwa likichunguzwa vikali katika kashfa inayomhusu mtangazaji wake wa zamani Jimmy Savile kwa madai ya kuwadhalilisha watoto.
Kipindi hicho cha Newsnight kinadaiwa kuacha kwa makusudi kutangaza habari ya uchnguzi kuhusiana na kashfa ya Bwana Savile.
Wakati wa kutangaza kujiuzulu Jumamosi,usiku Bwana Entwistle alisema "ilikuwa ndilo jambo la heshima kwangu kulifanya".
Akisimama kando yake Mwenyekiti wa BBC Trust, Lord Patten alisema " huu ulikuwa moja wapo ya usiku wa majozi katika maisha yangu ya umma".
"Muhimu kwa BBC ni jukumu lake kama chombo cha habari kinachoaminika"
"Kama Mhariri Mkuu wa shirika hili la habari, kwa heshima kubwa George amehiari kujiuzulu kutokana na makosa yasiokubalika - uanahabari mbovu ambayo umezua malalamiko mengi".

No comments:

Post a Comment