Pages

Pages

Thursday, November 8, 2012

FABAK FASHION YALETA ONYESHO LA KHANGA ZA KALE


Mama wa Mitindo nchini Tanzania, Asia Idarous kupitia Kampuni yake ya Fabak Fashions wanakuletea onyesho kubwa la Khanga za Kale litakalofanyika Novemba 23, 2012 katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam.

Onyesho hili kubwa ambalo limekuwa likifanya vizuri kwa takribani miaka minne sasa na kupata mafanikio makubwa ndani na nje ya Tanzania hasa katika nchi ya Marekani, litawakutanisha wabunifu zaidi ya 30 kutoka sehemu mbali mbali ambao nao wataonyesha mavazi yao waliyoyabuni.

Watu Maarufu hapa nchini watapanda jukwaani siku hiyo kuonyesha Mavazi ya Khanga za Kale kutoka kwa Mama wa Mitindo, Asia Idarous Khamsin ambapo fedha itakayopatikana kutokana na onyesho hilo imepangwa kupelekwa kwenye Kituo cha Kulea watu walioathirika na Madawa ya Kulevwa kilichopo Kikale Wilayani Rufiji, Mkoani Pwani.

No comments:

Post a Comment