Pages

Pages

Wednesday, November 7, 2012

VIGEZO VYA SHINDANO LA UNIQUE MODEL HADHARANI

Shindano la kumsaka mwanamitindo kumsaka mwanamitindo bora wa kike wa mwaka mwenye kipaji cha kipekee katika sanaa ya mitindo nchini Tanzania limechukua sura mpya baada ya kutangazwa kwa vigezo vya kujiunga na ushindi wa shindano hilo.
Akiongea chombo hiki mkurugenzi wa shindano la unique model Bw.Methudelah Magese amevitaja vigezo hadharani ili wananchi waelewe ni mwanamitindo wa namna gani anaetafutwa ili kuleta maana halisi ya jina la shindano hilo.
Vigezo vya kujiunga na ushiriki washindano hilo :-
                         (ii)     VIGEZO VYA KUSHIRIKI UNIQUE MODEL
·         Urefu usiopungua futi 5.8 na kuendelea.
·         Sura na  Umbo lenye mvuto wa kiuanamitindo.
·         Mvuto katika picha.
·         Uraia wa nchi yoyote.
·         Rangi ya ngozi na iwe asilia.
·         Umri wa miaka 18-25.
·         Tabia njema na muonekano wa heshima.
·         Uchangamfu,Uwezo wa kutambua mambo mbalimbali na kujieleza.

                    (iii)    VIGEZO VYA KUMPATA MSHINDI
              Jumla ya alama ni 100 na zimegawanyika kama ifuatavyo;-
·         sura na umbo lenye mvuto wa mwanamitindo. (Alama 30).
·         Uwezo wa ziada wa kutembea miondoko ya kimaonyesho ya nguo.(Alama 30).
·         Uwezo wa kutambua mambo mbalimbali na kujieleza (Alama 20).
·         Kujiamini na uchangamfu jukwaani.(Alama 10)
·         Nidhamu. (Alama 10)

 
Pia vigezo vya mshiriki kuwa mshindi lazima akidhi vigezo vifuatavyo na Jumla ya alama ni 100 na zimegawanyika kama ifuatavyo;-
Jumla ya majaji watatu watakaokaoteuliwa  watapewa semina elekezi na mratibu wa basata  namna ya utoaji alama kwa usahihi na kuzingatia haki ya kila mshiriki kwakua shindano hili lita kuwa wazi katika kuhakiki haki inatendeka  sawa na ubora wa mwanamitindo alivyo , alisema magese.
Hii ni hatua ya kipekee kwa waandaji wa mashindano kuwa wazi namna ya utoaji alama na kumpata mshindi kwakua itatoa mawazo tata na dhana potofu  ndani ya vichwa vya  wadau  wa tasnia ya mitindo.
Wito umetolewa kwa makampuni kujitokeza kudhamini shindano hili ambalo litaleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya mitindo nchini Tanzania ikiwemo kutoa ajira kwa mabinti zetu amabao wanachipukia katika fani hii,pia wabunifu wakubwa kwa wadogo wameombwa kutumia fulsa hii kujitangaza kwa kuwavalisha wanamitindo hao siku ya fainali ambapo inatizamiwa wabunifu wengi kujitokeza.
Pia wanamitindo wote wenye sifa na ndoto zakuwa wanamitindo maarufu kwa kukuza kipaji wameombwa kujitokeza kwa wingi siku ya tarehe 18/11/2012 saa nne asubuhi katika usaili pale Lamada  apartments & hotel iiyomo maeneo ya msimbazi center jijini dar.
Taji la unique model linashikiliwa na mwanamitindo Asia Dachi ambapo alikabidhi kwa mshindi wa mwaka huu unique model of ayear 2012 mwishoni wa mwezi desemba.
Unique model 2012 imedhaminiwa na Giraffe ocean view hotel,Dtv,Gazeti la Tanzania Daima,mashujaa Investment ltd,
Sophernner Investment co ltd,K.d.surelia,young don records,Kiu investment ltd,Oriental bureau de change,,J’s professional ltd,Lamada apartments hotel,T-moto Entertainment,wajanja club blog,Jiachie blog,mtaa kwa mtaa blog ,Michuzi blog na Unique entertainment blog.

No comments:

Post a Comment