Pages

Pages

Thursday, December 6, 2012

NJAA MBAYA,MWINYI AMLAMBA MIGUU JIDE

Katika kile kinachoonekana kama maisha kuanza kumpiga aliyekuwa muimbaji wa Machozi Band, Mwinyi Goha baada ya kuitosa, inadaiwa kuwa amempigia magoti Lady Jay Dee na kumuomba arudi kuendelea na kazi kwenye bendi hiyo.
Mwinyi alijiondoa Machozi Band katikati ya mwaka huu kwa madai ya kuchoshwa na uongozi wa kibabe, dharau na ubabaishaji wa wamiliki wa bendi hiyo.

 Pia alimshutumu Jaydee kwa kuwa na roho mbaya ikiwa pamoja na kumlipa ujira mdogo ambao nao alikuwa akipewa kwa masimango.

Na sasa Kupitia Facebook, Lady Jaydee amesema muimbaji huyo ameomba msamaha na anataka arejee kuendelea na kazi.

“Nadhani wote mnamkumbuka Mwinyigoha, aliekuwa MACHOZI BAND kitambo. Baada ya yote yaliotokea na mlioyasikia anataka kurudishwa kundini, Naomba mvae kiatu changu…, Je ingekuwa wewe ni JIDE ungemsamehe na kumrudisha tena kazini?? Jiweke kwenye nafasi yangu unipe jibu,” ameandika Jide.

Kutokana na maelezo hayo bado hatma ya Mwinyi Goha kurudishwa kwenye bendi hiyo ipo mikononi mwa mashabiki wa Lady Jaydee ambao wengi wamemshauri amsamehe.

No comments:

Post a Comment