Pages

Pages

Thursday, February 28, 2013

SHAA: SINA MAPENZI NA MASTER J

Shaa na Master J.
Hii interview ya Shaa kwenye Leo Tena ya Super Brand Clouds FM......

Ni kuhusu alichosema kuhusu taarifa za uhusiano wake na Producer Legend Tanzania Master J, ilikua ni interview ambayo hata mimi nilienjoy kuisikiliza manake Dina Marios na Shaa na wengine waliokuwepo studio walikua wamechangamka sana alafu Shaa alijiachia vizuri pia.
 
Alichojibu Shaa kwenye maswali ya ndio au hapana ni hapana, akisema “Ndugu mtangazaji hapana, hatuna uhusiano wowote”

Kwenye mstari mwingine Shaa alisema mpenzi wake atatambulika baada ya wazazi wake kumfahamu na kupokea mahari, baada ya hapo sasa kadi za mwaliko ndio zitaweka ukweli ambao wengi wanataka kuujua.

Basi baada ya kusoma hii stori ya Shaa natumia nafasi hii kukualika kuisikiliza hii hit song ya Promice ambayo iliandikwa na Barnaba Boy, support cha home.

No comments:

Post a Comment