Pages

Pages

Tuesday, March 5, 2013

KIJANA ACHARANGWA MAPANGA AKITOKA KUJIRUSHA USIKU

Kijana  Godfrey Masharo  mkazi  wa mjini Iringa  akivuja damu  baada ya  kuchomwa na kitu chenye ncha kali kifuani na watu  wasiofahamika  usiku  wa jana  wakati akitoka  kujirusha disco 

WATU  wasiofahamika   wamemvamia na  kumchoma  na kitu  chenye  ncha kali  kifuani mkazi  wa mjini Iringa Godfrey Masharo (pichani) .

Tukio hilo  limetokea jana usiku majira ya saa 11 alfajiri  wakati  kijana  huyo akitoka  kujirusha katika  kumbi  za starehe mjini  hapo.

Akizungumza kwa  tabu na mtandao huu  kijana  huyo anadai kuwa watu hao  watatu ambao hawafahamiki  kwa majina  walimvamia na kumchoma na kitu hicho chenye ncha kali kifuani na kukimbia .


Alisema  kuwa  tukio  hilo  limetokea eneo la Miyomboni barabara  kuu ya Iringa -Dodoma jirani na jengo la Hazina Ndogo ya  mkoa  wa Iringa .
Hata  hivyo  alisema  kuwa  msaada  wake  ulitoka kwa  wasamaria  wema ambao  walimkuta  eneo hilo akiwa ameanguka kwa  kupoteza fahamu na kukimbizwa  katika  kituo cha polisi kabla ya  kupelekwa Hospitali ya  rufaa ya mkoa  wa Iringa kwa matibabu  zaidi .
Umeona kifuani.....ni hatari sana

No comments:

Post a Comment