Pages

Pages

Tuesday, June 11, 2013

HALI YA RAIS WA KWANZA WA AFRIKA YA KUSINI NELSON MANDELA BADO NI TETE HOSPITALINI

Rais mstaafu wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela, akisaidiwa kutembea na Rais Jacob Zuma (kushoto) na mkewe wa zamani, Winnie Mandela (kulia). Imeelezwa hali ya Rais huyo mstaafu bado ni tete akiwa amelazwa Pretoria.
RAIS mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela, angali katika hali mbaya ingawa imeweza kudhibitiwa huku akiwa amelazwa katika hospitali moja mjini Pretoria.
"mzee Mandela yuko hospitalini na hali yake bado haijabadilika.''
Maombi dhidi yake yamekuwa yakifanywa makanisani kote nchini Afrika Kusini kumuombea Mandela ambaye anatibiwa kwa ugonjwa wa mapafu.

Bwana Mandela, mwenye umri wa miaka 94, alipelekwa hospitalini mapema Jumamosi , ikiwa ni mara ya tatu kulazwa hospitalini mwaka huu.


Picha ndogo (kushoto) Mzee Mandela akifurahia jambo na watoto nyumbani kwake hivi karibuni.
Kwa mujibu wa duru za urais, Mandela amekuwa akiugua kwa muda mjini Johannesburg baada ya kukumbwa tena na ugonjwa wa mapafu.

Alilazwa hospitalini baada ya hali yake kuwa mbaya zaidi mnamo Jumamosi.
Kwa mujibu wa taarifa za urais, Rais President Jacob Zuma, amerejelea wito wake kwa watu nchini Afrika Kusini kumuombea Madiba wakati huu anapougua.
Lakini mwandishi wa BBC mjini Pretoria, Karen Allen, anasema kuwa kuna matumaini amdogo kuwa Mandela aliyeongoza vita dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi, huenda kupona.
Anasema kuwa wengi walipata matumani baada ya bintiye Mandela Zindzi, kusema kuwa babake yuko salama na kuwa anaendelea kupata nafuu.

Mkewe Mandela Graca Machel, alifutilia mbali, ziara yake mjini London Jumamosi ili kuwa kando ya mumewe.

Mandela alikuwa Rais wa Afrika Kusini kati ya mwaka 1994 hadi 1999. 

Alifungwa jela miaka 27 na anaaminika kuwahi kuugua ugonjwa wa mapafu alipokuwa akifanyishwa kazi ngumu katika machimbo ya mawe akiwa jela.


''Rais huyo wa kwanza wa Afrika ya Kusini Nelson Mandela, aliyezaliwa Julai 18, 1918 Mvezo, nchini Afrika ya Kusini, jana aliliripotiwa na baadhi ya mitandao ya Kijamii kuwa amefariki dunia,

No comments:

Post a Comment