Pages

Pages

Tuesday, June 18, 2013

LUCY CHARLES NDIYE REDDS MISS MWANZA 2013


 Redd's Miss Mwanza 2013, Lucy Charles akipozi kwa picha mara baada ya kuvikwa taji hilo. 
Kinyanganyiro cha kumtafuta mnyange wa mkoa wa Mwanza kwa mwaka 2013, kiliteguliwa usiku wa ijumaa baada ya Mrembo Lucy Charles msomi wa chuo kikuu cha mtakatifu Augustino, kuwabwaga warembo wengine 13 waliojitokeza.
Nyota ya mrembo huyo ilianza kuonekana mapema, katika mavazi yote aliyovaa, lakini zaidi aliwapagawisha mashabiki wa urembo waliofurika katika ukumbi wa Yatch club baada ya kujibu swali kwa ustadi lililouliza Ni changamoto ipi kubwa walionayo vijana wa leo.
Mshindi wa pili katika shindano hilo ni Judith Josephat na mshindi wa tatu ni Suzan Ikombe.
Washindi hao watawakilisha mkoa wa mwanza katika shindano la kanda mwishoni mwa mwezi huu.
 Redd's Miss Mwanza 2013 Lucy Charles (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Judith (kushoto) pamoja na mshindi wa tatu Suzan Ikombe.
 Vazi la Ubunifu
Kivazi cha Ufukweni

No comments:

Post a Comment