Pages

Pages

Thursday, June 13, 2013

MISS MWANZA 2013 WATEMBELEA WATOTO YATIMA NA KUTOA ZAWADI

Mmona kati ya washiriki wa kinyang'anyiro cha kumsaka Miss Mwanza akionyesha ishara ya amani katika flash ya kamera ya blogu ya G. Sengo ikiwa nisehemu ya kuadhimisha siku ya kimataifa kupinga ajira kwa watoto ambapo warembo hao walitembelea kituo cha Kuleana jijini Mwanza na kutoa vyakula, sabuni, madaftari, kalamu na vihusishi vingine muhimu kwa maisha ya kila siku.
Mratibu wa Miss Mwanza 2013 Muhkis Mambo amesema kuwa nia na madhumuni ya menejimenti yake kuwaleta warembo hao hapa ni kuwajengea uwezo katika kuielezea jamii juu ya changamoto zinazowakabili watoto wa mitaani kwa wao kuzungumza na watoto wenyewe halikadhalika kujionea uhalisia.
Edna ambaye ni mmoja wa washiriki wa Redds miss Mwanza 2013 akiwa kwenye poz na wakali wa soka wanaounda timu ya watoto wanaoishi mazingira magumu Mwanza kituo cha kuleana.
Everlyne ambaye ni mshiriki wa Redds miss Mwanza 2013 akitoa neno la shukurani kwa wadau wa kituo hicho kuwapatia nafasi kujumuika nao kujifunza kwa uhalisia maisha wanayoishi.
Sabuni zilitolewa kwa kituo cha Kuleana.
Ili kuimarisha usafi zaidi.
Elimu ni muhimu na hapa ni makabidhiano ya madaftari.
Chakula nafaka ya maharagwe kikitolewa.
Daftari ndugu yake kalamu!!
Nafaka.
Makabidhiano ya Chakula (mchele).
Picha ya warembo wa kinyang'anyiro cha Redds Miss Mwanza 2013 na baadhi ya vijana wa kituo cha Kuleana.


'Wazazi nipendeni'
Pia warembo walipiga picha ya kusapoti michuano ya Kombe la dunia kwa watoto wa mitaani ambapo Tanzania ni moja kati ya nchi za Afrika zitakazoshiriki michuano hiyo itakayofanyika 2014 nchini Brazil.

No comments:

Post a Comment