Pages

Pages

Sunday, July 7, 2013

AJALI BASI LA SUMRY LAUWA WATU TISA



Basi la kampuni ya Sumry limetumbukia mtoni na kuua watu tisa na kujeruhi wengine hamsini na tatu.

Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Sitalike wilaya ya Mlele mkoani Katavi

Tukio hilo la kusikitisha lilitokea saa sita usiku kuamkia Julai 5, 2013 basi hilo lilipokuwa likitokea mjini Sumbawanga kuelekea Mpanda mkoani Katavi likiwa na abiri waliokuwa wametoka Mbeya.
 Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Katavi Emanuely Nnley alisema jana kuwa ajali hiyo ilihusisha basi aina ya Nissan Diesel lenye namba T909 AZT mali ya kampuni ya Sumry lililokuwa likiendeshwa na dereva aliyetajwa kwa jina na Stephano Chimane maarufu kwa  jina la Ntungu

Alisema basi hilo lilipofika katika daraja hilo lenye kona kali na mteremko,  dereva wake alishindwa kulimudu na kulenga daraja hali iliyosababisha tairi za nyuma kupanda juu ya ukingo na kutumbukia mtoni ambapo dereva wa basi hilo aliweza kutoka na kukimbilia kusikojulikana ...

Mkuu wa mkoa wa Katavi Dr Rajabu Rutengwe alitoa rambi rambi kwa wafiwa wote na kuwapa pole wahanga wa ajali hiyo mbaya kutokea tangu mkoa huo uanze.

No comments:

Post a Comment