Pages

Pages

Friday, July 5, 2013

NDOYA YA DIAMOND NA PENNY IMEIVA

 Diamond & Penny
SIYO siri kwamba wapenzi wasio na kificho, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Penny Mungilwa wana malengo ya kuja kuishi kama mke na mume lakini maajabu ni namna mwanamuziki huyo alivyopanga sherehe ya ndoa yao iwe siku ikifika. 
 
Akizungumza na gazeti la Ijumaa hivi karibuni, Diamond alisema kuwa yamekuwepo maneno ya chinichini kuwa ameshatoa mahari na siku si nyingi ataingia kwenye maisha ya ndoa ila ukweli ni kwamba kila kitu kinafanyika kwa umakini na mashabiki watajulishwa hatua kwa hatua.
  
“Suala la ndoa yangu nalifanya kwa umakini sana, watu wawe na subira tu ila wanachotakiwa kujua ni kwamba nina plani za kuifanya sherehe ya ndoa yangu kwenye Uwanja wa Leaders Club, pale Kinondoni na watu wataingia kwa kiingilio kisichopungua shilingi elfu kumi (10,000). Itakuwa ni ndoa ya Wasafi bana,” alisema Diamond.

No comments:

Post a Comment