Pages

Pages

Saturday, October 12, 2013

HAUSIGELI AMNYONGA MTOTO WA BOSI NA KUITUPA MAITI YAKE KWENYE DIMBWI LA MAJI MACHAFU HUKO KIBAHA

NI ukatili uliopitiliza! Hausigeli aliyejulikana kwa jina moja la Ester (14) yupo matatani kwa madai ya kumuua mtoto Arafat Allan (3) kwa kumnyonga shingo na kumpiga na kitu kizito kichwani kisha kuutumbukiza mwili wake kwenye dimbwi la maji machafu, Risasi Jumamosi limekamata tukio zima.
Tukio hilo lilijiri Jumapili iliyopita Mailimoja, Kibaha mkoani Pwani ambako marehemu alikuwa akiishi na wazazi wake.
Akizungumza kwa uchungu, mama mzazi wa mtoto huyo, Zakia Peter ambaye amelazwa katika Zahanati ya Kellen kutokana na mshtuko wa kifo cha mwanaye, alisema siku ya tukio, hausigeli huyo aliyekuwa na siku mbili tangu aanze kazi aling’ang’ania kutumwa sokoni saa mbili asubuhi ambapo alimkubalia na kumuagiza mboga.

AONDOKA NA MTOTO
Bila mwanamke huyo kujua, msichana huyo alimpitia Arafat kwa jirani alikokuwa akicheza na wenzake na kuondoka naye kwa madai anamsindikiza.
Nilipoona muda unasonga mbele bila hausigeli kurudi na mtoto nilianza kuwatafuta,” alisema mama wa marehemu.
Akasema aliwatafuta kwa muda mrefu bila mafanikio mwishowe yeye na majirani zake wakaenda kutoa taarifa polisi na kufunguliwa jalada la kesi KB/RB/1154/2013 TAARIFA.

HABARI ZASAMBAA MAITI YA MTOTO KUONEKANA KWENYE DIMBWI LA MAJI
Mama wa marehemu aliendelea kusema kuwa zoezi la kumsaka msichana huyo na mtoto wake liliendelea mpaka Jumanne iliyopita ambapo habari zilisambaa kwamba kuna maiti ya mtoto wa kiume  imekutwa ikielea kwenye dimbwi la maji machafu linalotumika kumwagilia bustani za mboga maeneo hayo.
Niliondoka na ndugu wengine hadi kwenye dimbwi hilo! Nilipata mshtuko mkubwa kukuta maiti ya mtoto anayeelea ni ya mwanangu Arafat,” alisema huku machozi yakimtoka.

MADAKTARI WAANIKA RIPOTI YA UCHUNGUZI
Baada ya hapo, mwili huo ulipelekwa katika Hospitali Teule ya Tumbi, Kibaha ambapo madaktari waliufanyia uchunguzi na kubaini kuwa marehemu alinyongwa shingo na kupigwa na kitu kizito kichwani hali iliyomsababishia mauti.

No comments:

Post a Comment