Pages

Pages

Wednesday, November 13, 2013

BODABODA YASABABISHA AJALI KWA CHALZ BABA


Kiongozi wa Bendi ya Mashujaa Musica, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’juzikati alipata ajali ya pikipiki  na kumsababishia majeraha sehemu mbalimbali za mwili wake.
Chanzo cha habari hii kilifunga safari hadi nyumbani kwake Mwananyamala, Dar kumjulia hali ambapo alisema tukio hilo lilitokea katikati ya wiki iliyopita, Ubungo baada ya kugongwa na gari kwa nyuma. 
“Nilikuwa natokea Kimara, nikiendesha pikipiki yangu. Si unajua tena ile barabara ipo kwenye matengenezo kwa hiyo
vizuizi ni vingi njiani. Ghafla nilishangaa pikipiki ikigongwa kwa nyuma, nikaanguka.

“Namshukuru Mungu maana mazingira niliyopata ajali ni mabaya sana isitoshe unajua pindi upatapo ajali kuna wengine wanakuja
kukusaidia na wengine ni wezi lakini sikuibiwa kitu.

“Nimeumia mkono, kiuno, mguu mmoja wa kushoto na maumivu kwa ndani lakini hakuna sehemu niliyovunjika,” alisema Chaz Baba.

No comments:

Post a Comment