Pages

Pages

Saturday, May 24, 2014

BASI LAUWA MTU MMOJA WILAYANI KOROGWE

Basi la abiria mali ya kampuni ya CHAKITO LONG WAY namba T354 ARK linalofanya safari zake kati ya jiji la Arusha na jiji la Dar es salaam limemgonga mtoto aliyekuwa akiendesha baiskeli na kumuua palepale baada ya kumuumiza vibaya wilayani Korogwe. Kwa mujibu wa shuhuda wetu mtoto huyo amegongwa na basi hilo alipokuwa akivuka barabara na basi hilo ambalo lilikuwa katika mwendowa kasi kuelekea jijini Dar es salaam.
Maiti ya kijana huyo ambaye hakufahamika jina lake mara moja
Katika ajari nyingine zaidi ya abiria 50 waliokuwa wakisafiri na basi la MAJINJAH SPECIAL  ambalo hufanya safari zake kati ya mikoa ya Dar es salaam na Mbeya wamenususrika kufa baada ya basi lao  kuacha njia na kwenda kutumbukia katika korongo mjini Iringa maeneo ya Mafing leo asubuhi  lilipokuwa likiktokea mjini Mbeya kuelekea jijini Dar es salaam . Ajari hiyo imetokea asubuhi ya leo na chanzo chake ni kufeli kwa breki katika basi hilo.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu hakuna aliyepoteza maisha katika ajari hiyo na basi lilitolewa na kuendelea na safari yake ya Dar es salaam. 

No comments:

Post a Comment