Pages

Pages

Saturday, May 24, 2014

MBUNGE VICKY KAMATA AUGUA GHAFLA NA KULAZWA HOSPITALINI, ALIKUWA AFUNGE NDOA LEO

Mbunge Vicky Kamata akiwa amelazwa Hospitali ya Tabata General, Dar es Salaam jana. Picha na Florence Majani  
---
Ni matukio nadra kutokea katika maisha, lakini haya ndiyo yaliyomkuta Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Vicky Kamata, baada ya kuugua ghafla saa 36 kabla ya harusi yake.

Kuugua kwa bibi harusi huyo mtarajiwa, kumezua gumzo katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma na maeneo mengine nchini, kutokana na kile kilichoelezwa kwamba harusi hiyo ilipangwa kuwa ya kifahari ikitarajiwa kutumia Sh96 milioni

Kamata ilikuwa afunge ndoa leo katika Kanisa Katoliki Parokia ya Bikira Maria Mama wa Mkombozi, Sinza Dar es Salaam na tayari kadi za mialiko zilishasambazwa kwa watu mbalimbali wakiwamo wabunge.

Habari za kuugua ghafla kwa mbunge huyo ambaye pia ni msanii wa muziki aliyetamba na kibao chake cha ‘Wanawake na Maendeleo’ zilianza kuzagaa kwa kasi juzi jioni nchini.

 Kamata ambaye pia ni mtetezi wa haki za wanawake,  aliugua usiku wa kuamkia jana na kupelekwa katika Hospitali ya Tabata General, iliyopo Segerea ambapo amelazwa.

“Niliugua tumbo ghafla, nilipata maumivu makali sana nikampigia daktari wangu na nilipomweleza jinsi ninavyojisikia, aliniambia niende hospitali haraka na kutokana na hali ilivyo, waliamua nilazwe,” alisema Kamata akiwa kitandani katika hospitali hiyo.

Kamata alifafanua kuwa, pamoja na mambo mengine, hali yake ya ujauzito imekuwa ikimsumbua na kuchangia yeye kulazwa kwa mara ya pili sasa katika kipindi cha wiki mbili. Mbunge huyo ambaye alitakiwa kufunga ndoa leo, alisema kuwa kutokana na maradhi hayo, haelewi hatima ya ndoa yake, ingawa wanafamilia na wanakamati wanaendelea na mipango ya harusi kama ilivyopangwa

No comments:

Post a Comment