Pages

Pages

Thursday, May 29, 2014

RAY NA JB PACHIMBIKA!...KUONESHANA UMWAMBA


Wasanii wakongwe wa filamu nchini, Jacob Stephan aka JB pamoja na Vicent ‘Ray’ Kigosi wanaandaa filamu nchini Uturuki itakayoonesha nani yupo juu zaidi kati yao.Akizungumza na Bongo5 jana, Ray amesema kuwa kila mmoja kati yao ana uwezo binafsi katika kazi ya filamu kwa hiyo filamu hiyo itaamuru nani yupo juu.“Mimi nilikuwa na movie na JB na tukaanza kushoot kule (Uturuki) lakini matokeo ya msiba wa Adam Kuambiana, tukasitisha zoezi na kuamua kutafuta tiketi kwa pamoja as a group za kuja kwenye msiba,lakini kwa bahati mbaya tukapata tiketi moja tu ambayo tukajadili kwa pamoja tukaona atuwakilishe JB,” alisema Ray  na  kuongeza
“Sisi tuna utaratibu wa kufanya kazi, zamani nilikuwa na utaratibu na marehemu Steven Kanumba ya kufanya kila mwaka sinema moja na kupimana ubavu kwenye filamu moja, kwahiyo baada ya kufariki Kanumba nikapanga na JB kila mwaka kutengeneza filamu moja ndio hiyo ambayo tumeianza na mambo ya misiba yakiisha tutarudi tena Uturuki kwenda kumalizia kazi.

"Hii ni mojawapo ya biashara na kuwatendea haki mashabiki wetu wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla kwa sababu tunapata comments nyingi sana kwenye Instagram, Facebook na Twitter kwamba hebu jaribuni kucheza filamu moja Ray na JB tumuone nani zaidi. 
"Nimecheza naye filamu nyingi  lakini kwa kipindi hiki kila mtu yupo juu. Ukiangalia JB amehit na mimi nipo juu pia kwahiyo tunahitaji kumtambua nani zaidi.”

KWA HABARI ZAIDI BOFYA OLDER POSTS

No comments:

Post a Comment