Pages

Pages

Wednesday, June 4, 2014

DEREVA NA UTINGO WAIBA MITUMBA YENYE THAMANI ZAIDI YA 100 ILIKUWA IKISAFIRISHWA KWENDA KONDO

Kamanda  wa  polisi mkoa wa Iringa akionyesha mitumba  iliyohifadhiwa katika nyumba  moja Nyololo baada ya kufaulishwa na dereva na utingo wake kisha lori kuchoma moto 

Mitumba  hiyo ikionekana kwa nje baada ya kujaa ndani ya nyumba hiyo kupita kiasi 
RPC Iringa Ramadhan Mungi akiangalia  mitumba  iliyohifadhiwa porini baada ya  kuporwa 
kamanda wa  polisi Iringa Ramadhan Mungi akimwonyesha mmiliki wa nyumba iliyohifadhi  mali  hizo za wizi kulia na dereva wa gari hilo mbele lenye namba  T 185 CJM ambalo  ndilo lilikuwa likisomba mali  hizo za wizi kutoka katika  lori lililochomwa moto 
Mwonekano wa lori hilo kwa ndani baada ya mali zote  kuhamishwa kwa  lengo la kuziiba 
Hili ndilo lori  lililokuwa na mali  hizo  chini kukiwa na ubichi wa mafuta  ya taa yaliyomwagwa ili  kulilipua lori hilo bila mafanikio 
JESHI la  polisi  mkoa  wa Iringa kupitia dhana ya polisi  jamii na ulinzi shirikishi  limefanikiwa  kukamata  mali za wizi zilizokuwa  zikisafirishwa kwenda nchi ya DRC Kongo zikiwa na thamani ya  Tsh milioni 100 pamoja na lori  lenye thamani  ya Tsh milioni 100 ambalo liliteketezwa kwa  moto kabla ya dereva na utingo wa  lori hilo  kulichoma moto kama njia ya kupoteza ushahidi.

Imedaiwa  kuwa  watu  zaidi ya 6  wanashikiliwa na  jeshi  hilo la polisi akiwemo  dereva  na utingo  wake ambao wanadaiwa  kuhusika na tukio  la wizi  huo.

Kamanda  wa  polisi mkoa  wa  Iringa Ramadhan Mungi  alisema  kuwa  tukio hilo  lilitokea juzi May 31 ambapo  askari  wa  doria  wilaya ya Mufindi  wakiwa katika shughuli   hiyo ya doria  walifanikiwa  kuliona  lori hilo  likiwa  limeegeshwa kando ya  barabara ya Iringa –Mbeya  eneo la Kinegembasi wilaya ya Mufindi  huku likiwa  limeteketea kwa moto katika kibini yake.

Alisema kuwa  watu hao waliteketeza lori lenye namba za usajili  T527 DPQ likiwa na tela lenye namba  T 974  EFE  aina ya  scania mali ya kampuni ya Dandu ambalo  walilikuta  likiungua   huku silizi  zake zikiwa  zimefunguliwa na  baada  ya uchungu wa awali  walibaini  kuwa lori hilo  lilikuwa limebeba mitumba na viatu  na baada ya msako  ndipo  walipofanikiwa  kukuta mitumba  hiyo  ikiwa imefichwa katika  nyumba moja kuukuu mali ya mama  Gray Mpinga  mwenyeji wa Maguhani Mufindi.

Alisema  kuwa mali  hizo ambazo ni mabelo ya mitumba na viatu  yalitoka Bandarini kwenda DRC  chini ya  dereva wa  lori hilo ni Enedia Christian (26) mkazi wa Mbeya  na utingo wake  Deus  Gendo (20) mkazi wa Mbeya .

Kamanda  Mungi  alisema kuwa utingo na dereva wa  lori hilo baada ya kufika kijiji  hicho cha Maguhani  walivunja kontena na  kushusha mali zote na kuzihifadhi katika  nyumba   hiyo kabla ya  kutafuta mteja na kisha  lori  kulichoma moto.

Alisema kuwa  baada ya  kufanya  wizi huo  walitoweka na simu zao kuzimwa na kutokana na jitihada za  jeshi la  polisi  kupitia mtandao wa kimawasiliano wa kuthibiti na wizi  wa mitandaoni  walifanikiwa  kuwanasa  watuhumiwa hao wakiwa kijiji cha Nyololo.

Mbali ya kuwakamata  dereva na  tingo  pia  polisi  wamekamata  watu  mbali mbali  wahusika  wa mtandao huo na kuendelea  kumsaka Masko Buhewa mkazi wa Nyololo kwa  kuhusika na umilikiwa wa mtandao huo .

No comments:

Post a Comment