Pages

Pages

Friday, September 26, 2014

AY KUACHIA VIDEO 2 MNAMO OCTOBA

Ambwene Yesaya aka AY ambaye ni mmoja kati ya wasanii wachache wa Tanzania ambao ujio wao huwa hautabiriki kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufanya mitindo mingi ya muziki amepanga kuwasapraiz mashabiki wake mwenzi ujio.
Mkali huyo ambaye hivi sasa anakinukisha na wimbo wake mpya ‘It’s Going Down’ aliourekodi California, Marekani akiwashirikisha Ms Trinity na Lamyia, alikuwa ndani ya The Jump Off ya 100.5 Times Fm jana na kueleza kuwa amepanga kuachia video mbili kwa mpigo mwezi ujao na kwamba moja kati ya video hizo ni It’s Going Down na nyingine itakuwa surprise.
“So la msingi ni hivyo, October video inatoka It’s Going Down na video nyingine ambayo ni surprise kwenu.” AY aliiambia The Jump Off.
“Nitachomoa mashine mbili, videos. So ni surprise kwenu..yes! October, hapa niko kwenye mchakato wa kufanya video na baada ya video nauhakika tutaendelea kupeperusha bendera ya muziki wa Bongo au East Africa kwa ujumla.” Ameongeza.

AY akiwa ndani ya The Jump Off na Jabir Saleh, kwa mbali ni DJ D Ommy.
Video zote zitafanyika Miami, Marekani mwezi ujao. Endelea kufuatilia hapa hapa na kupiti 100.5 Times Fm tutakujuza.

No comments:

Post a Comment