Pages

Pages

Friday, September 26, 2014

EVELYN BAASA NDIYE MISS TANZANIA PHOTOGENIC 2014

 

Miss Tanzania Photogenic 2014, Evelyn Baasa.


 Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya Miss Tanzania Photogenic 2014, wakiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa taji hilo, Evelyn Baasa (katiakti) jana. Wengine kutoka kushoto ni Nicole Sarakikya, Lilian Kamazima, Lilian Timothy na Dorice Mollel.



 Warembo wakilisakata rumba kabla ya kuatangozwa kwa matokeo hayo.


 Baadhi ya warembo wakipiga picha ya pamoja na mshindi huyo wa Taji la Miss Tanzania Photogenic 2014


Mlimbwende Evelyn Baasa (19) jana aliibuka kidedea kati ya walimbwende wenzake 30 na kutwaa taji la Miss Photogenic 2014.

Kwa kushinda taji hilo Baasa ambaye alinzania mbio za taji la Miss Tanzania katika Kitongoji cha Karatu na baadae kuingia Miss Arusha na Kanda ya Kaskazini amekuwa mrembo wa kwanza kuingia Nusu Fainali ya mashindano Miss Tanzania 2014.

Shindano hilo ni moja kati ya mataji matano ambayo yanashindaniwa na warembo hao ambapo washindi wake wanapata tiketi ya kuingia Nusu Fainali ya shindano hilo litakalo fanyika mapema mwezi ujao. 
 Brand new song

No comments:

Post a Comment