Pages

Pages

Sunday, June 12, 2011

ZANZIBA MUSIC AWARD ILIVYOFANA

Mbunge wa Jimbo la Uzini Zanzibar na Mkurugenzi wa Zanzibar Media Corporation Seif Khatibu kulia akiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi bora wa kike wa nyimbo za asilia Sada Mohamed mara baada ya kumkabidhi tunzo yake kwenye Zanzibar Music Award,zilizofanyika juzi mjini Zanzibar na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Mjumbe wa NEC Aisha Kigoda kulia akimkabidhi Tunzo msani bora chipukizi wa kike Sauna G kwenye Zanzibar Music Award,zilizofanyika juzi mjini Zanzibar na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Mwanamziki wa kizazi kipya Baby J akionysha Tunzo yake ya pili mara baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Zenj Fm.
Mwanamziki wa kizazi kipya Baby J akiwa ameshikilia Tunzo yake aliyejinyakulia kwenye Zanzibar Music Award 2011, kuwa mwanamziki bora wa kike wa muziki wa kizazi kipya ,zilizofanyika juzi mjini Zanzibar na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania,kulia ni Hagai Samson aliyemkabidhi tunzo hiyo.
Meneja wa Vodacom Tanzania kanda ya Zanzibar Mohamed Mansour kulia akimkabidhi Tunzo Mwanamziki bora wa kiume wa nyimbo za kizazi kipya Juma Twenty kwenye Zanzibar Music Award,zilizofanyika juzi mjini Zanzibar na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania.
Aaah tamaduni zetu za mwambao hatuziachi kata kidogo kwenye Zanzibar Music Award tunaburudisha.
Baadhi ya masharobaroz walioudhuria Zanzibar music award.


SIMBA YAINYUKA MOTEMA PEMBE 1-0

Mchezaji wa timu ya Simba Mussa Hassan Mgosi Mchezaji wa timu ya Simba akiwa amembeba mchezaji mwenzake Amri Kiemba mara baada ya kupachika goli la kwanza na la ushindi, katika goli la timu ya Motema Pembe kutoka DRC kwenye mchezo wa michuano ya Kombe la Shirikisho la CAF, uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jioni hii, goli hilo limefungwa kipindi cha kwanza dakika ya 20 ya mchezo huo mshabuliaji Mgosi aliipokea pasi nzuri kutoka kwa kiungo Mohamed Banka kufunga goli hilo pekee, hivyo Simba imefanikiwa kuwatoa "ulimi nje" wapinzani wao Motema Pembe ya DRC.
 
 
 
 
RAIS WA SOMALIA AFURAHIA KIFO CHA KIONGOZI WA AL QAEDA

Rais wa Somalia, Sheikh Sharif Sheikh Ahmed, ametoa maelezo zaidi kuhusu kuuawa kwa kiongozi wa Al Qaeda Afrika Mashariki, Fazul Abdullah Mohammed, ambaye alipigwa risasi mjini Mogadishu siku ya jumatano.
Sheikh Sharif
Rais wa Somalia
Rais wa Somalia alisema Marekani ilisaidia kuthibitisha utambulisho wa mtu huyo, na ukaguzi ulifanywa nje ya nchi.
Aliwaonesha waandishi wa habari, ile ambayo alisema, ni hati ya kuzaliwa ya Fazul Abdullah Mohammed, picha za familia yake, na ramani ya pengine malengo ya kushambulia mjini Mogadishu.
Mogadishu
Aliahidi kushambulia Mogadishu

Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Marekani, Hillary Clinton, ambaye yuko Tanzania - akitarajiwa leo kuweka shada la mauwa kwenye jengo la ubalozi wa Marekani, lililoshambuliwa kwa bomu na Al Qaeda mnamo mwaka wa 1998, kwenye operesheni, ambayo Marekani inasema, ilipangwa na Fazul Abdullah Mohammed.



TWAMGA PEPETA USIKU WA JANA
Bendi ya Muziki wa dansi ya The African Stars International wafunika usiku wa kuamkia leo kwenye ukumbi wa Mago Garden 'Twanga City' Kinondoni Jijini Dar es Salaam. leo mchana wako Mbalamwezi ambako watashirikiana na msanii Dully Sykes wakati usiku watakuwa TCC Chang'ombe. Hapa sijui nikwambie nini huyu dada anaonekana jinsi mzuka ulivyompanda.
Lilian Tungaraza 'Internet' hapa akiwa full mzukaaa.

No comments:

Post a Comment