Pages

Pages

Monday, September 12, 2011

DIANA JOHN: MREMBO MKALI MWENYE HAIBA

  Diana John ni mrembo ambae nyota yake imeanza kung'aa mwaka huu,ana umri wa miaka 21,kabila lake mrangi,elimu yake ni kidato cha nne,anapendelea makande,anapendelea kucheza muziki na kuogelea japo hawezi kuogeleana matarajio yake ni kujiendeleza kielimu zaidi.


REDD'S MISS ILALA YAFUNIKA MISS TANZANIA 2011
Meneja wa kinywaji cha Redds Victoria Kimaro akimpongeza mshindi wa Miss Tanzania (2011 to 2012)  ambae ni Redds Miss Ilala Salha Israel baada ya kuibuka mshindi
  
 Meneja wa kinywaji cha Redds Victoria Kimaro akipongezana na Mwandaaji wa Miss Ilala Jackson Kalikumtima

  
 Akifanya mahojiano huku pembeni yake akisindikizwa na mtaalamu wa mawasiliano wa kampuni ya Vodacom  Martina Nkuru


. Meneja wa kinywaji cha Redds akiingia ukumbini kabla ya kujua kuwa mrembo aliyebeba jina la Redds kuwa angeibuka na ushindi wa Miss Tanzania 
  Kama mnavyojua juzi kwenye shindano la Miss Tanzania 2011 washiriki watatu kutoka Redds Miss Ilala waliingia kwenye top 5 ambapo wawili kati yao waliingia top 3 na mmoja kunyakua taji la Miss Tanzania.
  Redds ilikuwa mdhamini mkuu wa mashindano ya kanda za Dar es Salaam zilizojulikana kama Redds Miss Ilala, Redds Miss Temeke na Redds Miss Kinondoni hivyo basi inajivunia ushindi huu wa kishindo kutoka kwenye moja ya kanda zake.
  Inachukua fursa hii kuwapongeza washiriki wote hususan Redds Miss Ilala Salha Israel ambaye ndiye Miss Tanzania 2011.
  Tunashukuru wanablogs kwa ushirikiano wao mkubwa tangu mwanzo wa mashindano kwenye vitongoji na kanda na mpaka kwenye mashindano ya taifa.

No comments:

Post a Comment