Pages

Pages

Saturday, September 10, 2011

WAREMBO WA MISS TANZANIA WATOANA MACHO KAMBINI LEO

  Joto la nani kutangazwa mshindi wa taji la Miss Tanzania limepanda kiasi kwamba washiriki wako roho jujuu kambini hapo.
  Ukweli bila pingamizi ni kwamba Mrembo Salha Israel ndiye anaekimbiza warembo hao 29 akiwakilisha kanda ya Ilala ambapo washiriki wengine Kama Alexia na Jennifer wamekuwa tishio katika shindano hili,ndiyo wanaotegemewa kufanya vema zaidi leo usiku.SHANGILIA ILALA ZONE LEO USIKU.
Salha Israel... Our Dream 2011.
               Jennifer Kakolaki.
                Alexia Williams.
uniqueentertz blog imekuwa sambamba na warembo hawa kuwapa sapoti ya kutosha mwanzo mwisho.



MELI YAZAMA ZANZIBAR MAMIA WAPOTEZA MAISHA
 zaidi yawatu 600 wahofiwa kufa maji,jeshi la uokoaji likitoa msaada wa kuwaokoa abiria walozama.
Mamia ya watu wanahofiwa kufariki dunia baada ya feri kuzama katika pwani ya kisiwa cha Zanzibar nchini Tanzania ikiwa imewabeba zaidi ya watu mia tano.
Zaidi ya watu arobaini na tatu wameaga dunia katika mkasa huo , mmoja wa mawaziri katika kisiwa hicho kinachojitawala amesema.
Takriban watu 260 wameripotiwa kuokolewa
Feri hiyo MV Spice Islander ilikuwa ikisafiri kati ya kisiwa kikubwa zaidi cha Unguja ikielekea Pemba ambacho pia ni kisiwa cha Zanzibar.
Hadi kufikia sasa tumeopoa miili 43, lakini tumewaokoa manusura 259
Mohammed Aboud, waziri anayehusika na maswala ya dharura Zanzibar.
" ," amesema Mohammed Aboud, waziri wa Zanzibar anayehusika na mikasa. Ameongeza kuwa 40 kati ya wale waliookolewa walikuwa na mejeraha mabaya.


             PICHA ZETU
Mtoto Jacky akipozi kwenye picha nyumbani kwa babu yake mzee wilison Magese.
Yason leo tunywe ngapingapi?...aaah Makoye mi moja tu leo..
          Dar inazidikuwa na majengo ya kisasa siku hadi siku vitu vipya vinaporomoshwa.
           "Dont hate me b'cause am beautiful" Miss kagera 2011,cocklate baby 
Biashara ya viatu meshamiri jiapanda ya barabara ya kawawa na Morogoro.


JE WAIJUA BUKOBA?
Katikati ya mji wa bukoba maeneo ya stendi kuu ya mabasi,bustani nzuri yenye nakish ya mwamba,ziwa na migomba.

 

AMWAGIWA TINDIKALI NA KUUNGUA VIBAYA MJINI IGUNGA

MFUASI wa CCM, Mussa Tesha (24) akiwa katika hospitali ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora, leo. Tesha ameungua usoni na sehemu kadhaa mwilini baada ya kumwagiwa tindikali usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana, ambapo inaelezwa kuwa walimwagia tindikali hiyo alipokuwa katika harakati za kubandika mitaani mabango ya mgombea wa Ubunge jimbo lgunga kwa tiketi ya CCM. Tesha alitarajiwa kuhamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Sala leo kwa gharama za CCM Kumekuwepo na kushutumiana kati ya vyama vya CCM na CHADEMA kutokana na matukio kadhaa ambayo yamekuwa yakitokea, hasa katika kipindi hiki cha Kampeni kuelekea uchaguzi mdogo wa Mbunge wa jimbo la Igunga, kufuatia kujiuzulu kwa mbunge wa zamani wa jimbo hilo Bw. Rostam Azizi Vyombo vya usalama na ulinzi vinatakiwa kuwa katika hali ya tahadhari na umakini mkubwa kwa muda wote wa kampeni za uchaguzi katika jimbo hilo, ili kudhibiti vitendo kama hivyo vinavyoweza kupelekea uvunjifu wa amani na utulivu katika kipindi hiki cha kampeni jimboni humo.
MFUASI wa CCM, Mussa Tesha (24) akiwa katika hospitali ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora, leo. Tesha ameungua usoni na sehemu kadhaa mwilini baada ya kumwagiwa tindikali usiku wa kuamkia leo na watu wasiofahamika , ambapo inaelezwa kuwa walimwagia tindikali hiyo alipokuwa katika harakati za kupandika mitaani mabango ya mgombea wa Ubunge jimbo lgunga kwa tiketi ya CCM. Tesha alitarajiwa kuhamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es Sala leo kwa gharama za CCM
Anayemtazama ni Daktari wa hospitali hiyo, Selemani Masinga.

No comments:

Post a Comment