Pages

Pages

Thursday, September 8, 2011

WAZIRI NUNDU AMTEUA DKT. KIJAZI KUWA MKURUGENZI MKUU WA HALI YA HEWA

 
Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu amemteua Dk. Agnes Lawrence Kijazi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)
Taarifa iliyotolewa jana katika vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Omari Chambo ilisema uteuzi huo umefanyika kwa kuzingatia sheria ya wakala wa serikali Na. 30 ya mwaka 1997 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 2009.
Aidha taarifa hiyo iliongeza kuwa kulingana na uteuzi huo Dk. Agnes Lawrence atachukua na kuitumikia nafasi hiyo kuanzia tarehe 06/09/2011 kwa kipindi cha miaka mitatu ambapo kitaisha tarehe 06/09/2014
Kabla ya kuteuliwa kushika wadhfa huo Dk. Kijazi alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.


WINEHOUSE ALILIPA PAUNI 150 KWA KISS MOJA
 Habari za kina toka magazeti ya udaku ya Uingereza kuwa Artist Amy Winehouse,inasemekana ameacha utajiri wa siri wa pauni milioni 2 za Uingereza.
 Pia inasemekana pindi demu huyu akimtaka mwanaume hugharamia mazima,kwani aliwahi kulipa pauni 150 za uingereza kwa kisi moja toka kwa mwanaume.

No comments:

Post a Comment