Pages

Pages

Wednesday, October 19, 2011

KANUMBA KUSHIRIKI MATEMBEZI YA HISANI NA MAMA SALMA KIKWETE

  Muigiza wa kimataifa Steven Kanumba ameafiki kuungana na mama Salma kikwete kuhamasisha uchangiaji wa fedha kwaajili ya watoto wenye kansa na watoto waishio na virusi vya ukimwi katika hospitali ya Mihimbili iliyopo jijini Dar,matembezi hayo yatafanyika tarehe 5 novemba mwaka huu huku yakisindikizwa na blast bend ya jeshi la polisi.
  Edge Eaqntertainment chini ya mkurugenzi wake Bw. Edwin Ngere ameiambia blogu hii kuwa matembezi yataanzia viwanja vya mnazimmoja hadi Moven Pick mbako ndiko kutakuwa na hafla ya kuchangisha pesa kwaajili ya watoto hao.
  Mbali ya hao watakuepo wake za mabarozi wa nchi zote na baadhi ya mawaziri wakiambatana na wanawake 100 wenye mafanikio nchini Tanzania ambao wote watatembea kwa pamoja kisha kusaidia watoto huku shughuli hiyo ikiratibiwa na mwanamuziki Stara Thomas.
  Pia matembezi haya yataingia mikoani jumla ya mikoa sita itashiriki kuchangia watoto wenye magonjwa ya saratani na washio na virusi vya ukimwi katika mikoa hiyo husika.
  Matembezi haya yamedhaminiwa na Moven Pick Hotel.CRDB Bank,fly 540,zizzou fashion,,clouds fm na Uniqueentertz Blog.
   


KUMEKUCHA MISS KAMPALA UNIVERSITY 2011 
 Baadhi ya washiri akiwa katika pozi la pamoja.NANI KUTWAA TAJI HILI JUMAMOSI HII?

 

No comments:

Post a Comment