Pages

Pages

Wednesday, November 30, 2011

MISS UTALII PACHIMBIKA MAMLUKI WATIMULIWA

 Bodi ya wakurugenzi ya Miss Tourism Tanzania Organisation, yenye dhima ya kikomo ya kuandaa na kuendesha mashindano ya Miss Utalii Tanzania,imeendelea na safisha safisha ya viongozi na waandaaji wababaishaji na mamluki,baada ya kuwafutia kuwatimua waandaaji wa Miss Utalii Dodoma, imemfukuza aliyekuwa mpiga picha wa mashindano hayo katika kamati ya Taifa ya Miss Utalii Tanzania, Shaabani Mpalule,kwa tuhuma za umamluki na hujuma za mashindano hayo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyo tolewa na Rais wa Mashindano hayo, Gideon Chipungahelo, sababu za kufukuzwa ikiwa ni mara ya tatu sasa,baada ya kuwa amefukuzwa mwaka 2008, na kurejeshwa mwaka 2011 mwanzoni na kufukuzwa mwezi July 2011, kisha akaomba msamaha na kurejeshwa mwezi septemba 2011 kwa majaribio.
Sababu za kufukuzwa ni pamoja na utovu wa nidhamu ulio tukuka,kokosa uaminifu, na umamluki wa kuhujumu shindano la Miss Utalii Tanzania. Baadhi ya utovu huo wa ni dhamu na maadili ni pamoja na tuhuma za kutaka kubaka washiriki, kuiba nyaraka za kampuni, kutumia jina la mashindano kujipatia huduma ,mali na hata fedha kwa maslahi binafsi. Kupigana na waandaaji na wanakamati kiasi cha kuharibu mali za watu na hoteli, kuiba mali za wajumbe na wanalamati wengine zikiwemo kamera na mashine za DVD.
Pia imethibitika kuwa ni mamluki ambaye anamaslahi na anatumiwa na waandaaji wa mashindano mengine hususani shindano la Miss Demokrasia ambalo,amekuwa akijaribu kuliandaa bila ya mafanikio, pamoja na hujuma nyingine amekuwa akisambaza mbalimbali za kutengeneza katika mitandao mbalimbali,wadhamini na hata baadhi ya vyombo vya habari ,kutishia warembo na hata kutoa vitisho mbalimbali kwa waandaaji wa ngazi za chini na wanakamati wengine. Aidha amekuwa kinara wa uvurugaji mashindano haya kwa kusambaza taarifa mbalimbali za kukashfu,kucha shindano na kuwachafua viiongozi ,washiriki,washindi na hata sanaa ya urembo na ustawi wa shindano hili na mengine nchini, Wakati wote akiwa mpigapicha wa mashindano haya amekuwa akitumia picha kuwatishia washiriki na kuwapa masharti ambayo ni kinyume cha maadili ili awepe picha. Wakati wote amekuwa na tabia za kutumia au kuweka maelezo tofauti na picha za matukio mbalimbali ya mashindano kwa lengo la kuchafua warembo na mashindano kwa ujuma.

  JERRY MURO YUKO HURU

Mwandishi wa habari aliepata misukosuko Jerry Muro akiongea na waandishi wa habari leo baada ya kuachiwa huru na mahakama ya hakimu mkazi Kisutu.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijijini Dar es Salaam imemwachia huru na kuwafutia mashtaka aliyekuwa Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Jerry Muro pamoja na washtakiwa wenzake wawili ambao ni Edmund Kapama na Deogratius Mgasa waliokuwa wakikabiliwa na kesi ya kuomba rushwa ya tsh.10 milioni.


BREAKING NEWS; MCHEKESHAJI O'NEAL AFARIKI DUNIA

Breaking News - Patrice ONeal died Monday night
Comedian Patrice O'Neal died Tuesday morning ... as a result of a stroke he suffered back in October ... this according to his friends at the "Opie and Anthony" radio show.

O'Neal had been a staple in the comedy world for years -- and performed at the "Comedy Central Roast of Charlie Sheen" back in September.

O'Neal was a regular guest on the "Opie and Anthony" radio show -- and appeared on several TV shows such as "Chappelle Show," "The Office," and "Tough Crowd with Colin Quinn."

Opie just tweeted, "Yes it's true that our pal Patrice O'Neal has passed away. The funniest and best thinker I've ever known PERIOD."

No comments:

Post a Comment