Pages

Pages

Thursday, November 10, 2011

WATANZANIA WAMECHOSHWA MISS TANZANIA KUSHIKA MKIA KILA MWAKA MISS WORLD

  Hivi karibuni mamilioni ya watu duniani ambao walishuhudia mashindano ya Miss world yakitimiza miaka 60 na fainal zake kufanyika London Uingereza na Kama kawaida Tanzania tulipeleka Mwakilishi wetu Salha Izrael, na Kilichotokea ni kile ambacho tumekizoea na Mwakilishii wetu akabaki kuwa mshiriki na sio mshindani, ni hadithi ambayo imezoeleka,
  Miss Venezuela, Ivian Lunasol Sarcos Colmenares,aliwashinda washiriki wengine kutoka nchi 113 na kutwaa taji hilo baada ya kuwaridhisha majaji katika mashindano hayo kwa kufanya vizuri katika categories zote starting with beach beauty, top model, talent, sports, and beauty with a purpose - where the contestants must demonstrate involvement in a charity project.
 Shindano la Miss Tanzania lina historia kubwa na inayovutia ambapo mshindi wa Kwanza kabisa anayetambulika alikuwa ni Bi Theresia Shayo ambaye alijinyakulia Taji hilo rasmi mwaka 1967, Shindano hilo lilipita kipindi cha kufungiwa na serikali mpaka mwaka 1994 pale akina Uncle Hashim Lundenga na kamati ya Miss Tanzania walipolifufua tena na kulijenga kulipa umaarufu mkubwa ulionao hivi sasa.       

Kuanzia mwaka huo ambako Aina Maeda alipata nafasi ya Kuiwakilisha Tanzania Miss world, Haijatokea mrembo wa Tanzania Kufanya vizuri katika mashindano ya dunia ukiondoa Mwaka 2005 ambapo mrembo Nancy Sumari aliweza Kunyakua taji la Miss Afrika kwa kufika Fainali ya top 7, darbase.com haitakuwa na fadhila kama haitotambua mafanikio mengi ambayo kamati ya Miss Tanzania imeyapata katika kipindi hicho, kubwa ikiwa ni kufanya Miss Tanzania kuwa shindano kubwa la urembo afrika mashariki na kati, uendeshaji wa ufanisi wa kamati pamoja na kufungua njia kwa warembo wengi ambao wamepata nafasi kupitia miss Tanzania, wengi wamepata kazi katika mashirika, wamefanikiwa katika fani ya modelling duniani na wamekuwa wakipewa zawadi ambazo zilianzia nyumba mpaka magari.
  Ni mafanikio makubwa yanayostahili kuthaminiwa na wote wanaopenda maendeleo,darbase.com kama mdau wa urembo chini Tanzania inatoa pongezi kubwa kwa Hashim Lundenga na timu yake kwa mafanikio hayo
Miss Tanzania kutokana na mafanikio yake imeweza kuvutia Makampuni makubwa hapa nchini kutoa udhamini wa uhakika kitu ambacho wenzetu Kenya na Uganda hawajaweza kukifikia, Akina Lundenga na Timu yake wamefanya kazi kubwa, hili hakuna ubishi.
  Kama ulipata nafasi ya kuangalia fainali za mwaka huu utagundua kuwa mashindano hayo yamebadilika sana, sio urembo pekee but it is beauty with purpose, Mashindano yamekuwa na vipengele vya beach beauty, top model, talent, sports, and beauty with a purpose - where the contestants must demonstrate involvement in a charity project.



 R&M RUN WAY FASHION SHOW IN NEW YORK

Pier 57 in New York City was star studded, thanks to a fashion show for the Versace for H&M x collaborative collection. Earlier, we showed you behind the scenes pictures of some items from the collection. Now we have pictures of the looks from the actual runway show!


 TETEMEKO LAPOROMOSHA HOTELI UTURUKI

Jengo lililoporomoka Uturuki
Waokozi wanajaribu kuwaokoa manusura waliokwama katika vifusi vya majengo baada ya tetemeko la ardhi la kipimo cha 5.7 kukumba mji wa Van, kaskazini mwa nchi ya Uturuki.  Majengo kadhaa yameporomoka wakati tetemeko hilo liligonga, ikiwemo hoteli moja la ghorafa sita. Takriban wafanyakazi 100 wa kutoa misaada na waandishi wa habari wanaaminika walikuwa wanaishi katika hoteli hiyo. Waandishi hao walikuwa katika eneo hilo kwa sababu ya tetemeko lingine lililokumba eneo hilo wiki mbili zilizopita, ambapo watu wasiopungua 500 walikufa. Baadhi ya waandishi waliokwama wamekuwa wakituma ujumbe mfupi wa simu ya mkononi wakiomba usaidizi. Akizungumza na BBC mbunge wa Uturuki, Nasmi Guhr, amasema '' Takriban majengo mengine 40 yameporomoka mjini Van na makundi ya waokozi wanajaribu kuokoa waliokwama''.

No comments:

Post a Comment