Pages

Pages

Friday, January 13, 2012

KATIBU MKUU WA NCCR AZOMEWA KIGOMA

Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila

KATIBU Mkuu wa NCCR- Mageuzi, Samwel Ruhuza juzi alilazimika kushuka jukwaani baada ya kuzomewa na wananchi wakati akihutubia mkutano wa hadhara wilayani Kasulu, mkoani Kigoma.

Ruhuza amepiga kambi mkoani Kigoma tangu Januari mosi mwaka huu, akiongoza kikosi maalumu cha viongozi wa chama hicho, kinachoendesha operesheni ya ufuatiliaji wa utekelezaji ahadi za wabunge na madiwani wake.


Rwehuza alikumbana na balaa hilo pale alipojaribu kuwaeleza wananchi hao juu ya uamuzi wa Halmashauri Kuu ya NCCR- Mageuzi, kumvua uanachama kada wa chama hicho ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila.

Operesheni ya viongozi hao mkoani Kigoma, ilianza siku siku chache baada Kafulila kuanza ziara mkaoni humo, kwa kile alichoeleza, kutembelea wapigakura wake, ambapo pamoja na mambo mengine, amekuwa akielezea hatma ya ubunge wake baada ya kuvuliwa uanachama Desemba 17 mwaka jana.

No comments:

Post a Comment