Pages

Pages

Monday, March 19, 2012

MAANDALIZI YA BONANZA LA VYOMBO VYA HABARI MBALIMBALI YANAENDELEA VIZURI

 MAANDALIZI kwa ajili ya bonanza la vyombo mbalimbali vya habari litakalofanyika Machi 24 mwaka huu ukumbi wa Msasani Beach Club, Dar es Salaam yanaendelea vizuri.
Tayari Kamati ya Maandalizi imeshatuma barua za mialiko kwa vyombo mbalimbali vya habari na naomba wote walialikwa wathibitishe haraka iwezekanavyo ushiriki wao kulingana na walivyojulishwa.

Pia Kamati ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), imeshafanya maandalizi ya burudani mbalimbali kwa ajili ya bonanza hilo, ikiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya, ambao bado tunaendelea na mazungumzo nao.

Tayari kamati imeshamalizana na bendi ya FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ kutumbuiza kwenye bonanza hilo linalodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL). 

Hivyo burudani itakuwa Wazee wa Ngwasuma na wasanii wa muziki wa kizazi kipya, ambao tutawatambulisha siku yoyote wiki hii kabla ya Alhamisi pamoja na mgeni rasmi.
Tunataka bonanza la mwaka huu liwe la aina yake kuanzia burudani, michezo na mambo mengine yawe ya aina yake. 

Bonanza litaanza saa tatu asubuhi hadi saa mbili usiku, ambapo baadhi ya michezo itakayoshindaniwa ni soka ya ufukweni, netiboli, wavu, mbio za magunia, mbio meta 100, kuruka kichura, kuvuta kamba, kucheza muziki na michezo.

 Tunaonya kuwa kampuni ambayo itashindwa kuthibitisha ushiriki wake mapema kwa michezo itakayocheza haitapangwa, hivyo tunaomba wahusika watilie mkazo jambo hilo.

No comments:

Post a Comment