Pages
BRAND NEW MUSIC
metty magese
Listen & Download
http://mdundo.com/a/32626
Tuesday, April 30, 2013
Sunday, April 28, 2013
ASNATH KUTOKA CHUO KIKUU MZUMBE ATWAA TAJI LA REDD'S MISS HIGHER LEARNING MOROGORO 2013
Mshindi wa Shindano la Redd’s Miss Higher Learning
Mkoa wa Morogoro, Anitha Mwakitwange kutoka Chuo Kikuu cha Mzumbe akipunga
mkono mara baada ya kuvikwa taji hilo usiku wa kuamkia jana katika shindano
lililofanyika Mjini Morogoro. Anitha aliwashinda warembo wenzake 10 aliokuwa
akiwania nao taji hilo.
Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro, Anitha
Mwakitwange(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mshindi wa pili Rosemary
Aloyce (kulia) na Mshindi wa Tatu Tarchisic Mtui mara baada ya warembo hao
kutawazwa kuwa ndio washindi wa Shindano hilo usiku wa kuamkia jana katika
shindano lililofanyika Mjini Morogoro. Anitha ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo
Kikuu Mzumbe aliwashinda warembo wenzake 10 aliokuwa akiwania nao taji hilo.
Majaji
wa shindano hilo wakiwa tayari katika meza yao kusubiri washiriki wa
Redd's Miss Higher Learning Morogoro kupanda jukwaani kuwania taji hilo.
Mashabiki
na wapenzi wa Sanaa ya Urembo kutoka Mkoa wa Morogoro na wengi wao
wakiwa ni wanafunzi kutoka Vyuo vya Mzumbe, SUA, Jordan, St Joseph na
MSJ wakisubiri kuanza kwa shindano hilo la Redd's Miss Higher Learning
2013.
Washiriki wa shindano la Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro
wakicheza show ya ufunguzi wa shindano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia jana
na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya Juu mkoani humo.
Mwakilishi wa Kamati ya Miss Tanzania ambaye ni Afisa Habari wa Kamati hiyo, Hidan Rico akizungumza machache.
Huyu alibuni vazi lake kwa Kitenge na makaratasi.
Huyu alitumia Majani ya mti wa Muashock...
Kiroba nacho kilichukua nafasi yake kwa mrembo huyu ....
Miss Higher Learning yeye aliamua kutumia majani ya maua kutengeneza kauni lake maridani la ubunifu.
Wapenzi wa sanaa ya urembo wakifuatilia kwa umakini onesho hilo.
Msanii chipukizi wa Mkoa wa Morogoro, ambaye ni mwanafunzi wa Chuo cha St Joseph ajulikanae kama Jose alitumbuiza..
Ulifika wasaa wa kivazi cha Ufukweni na kila mmoja alienda Mindu kuogelea kwa kivazi chake...
Huyu aliingia hivi katika maji...
Huyu alivaa hivi...
Ilikuwa ni raha kwa mashabiki usiku huo ndani ya Savoy mjini Morogoro...
Ilikuwa
ni shangwe kwa wapenzi na mashabiki wa sanaa ya urembo Morogoro hasa
meza hii ya Mzumbe ambayo ilishajua wazi kuwa taji ni lao mapemaaa...
Vazi la usiku lilipita na kisha tano bora ikatangazwa...
Warembo waliofanikiwa kuingia hatua ya tano bora ya
Redd’s Miss Higher Learning Mkoa wa Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja
maara baada ya kutwajwa wakati wa shindano hilo lilifanyika usiku wa kuamkia
jana na kushirikisha warembo 11 kutoka vyuo mbalimbali vya elimu ya Juu mkoani
humo. Kutoka kushoto ni Tarchisic Mtui, Rosmary Aloyce,Hellen Mhando, Tausi Idd
na Asnath Mwakitwange.
Washiriki wote ndio hawa hapa...
Mzee
wa Magube Gube!! Barnaba Boy aliwapagawisha vilivyo wapenzi wa sanaa ya
urembo hasa wanafunzi hawa kutoka vyuo mbalimbali vya Elimu ya Juu
Mkoani Morogoro.
Walijiachia vilivyoo...katika sho hiyo kali
Wednesday, April 24, 2013
MUIGIZAJI LULU MICHAEL KATIKA POZI TOFAUTI MWAKA 2013
Tuesday, April 23, 2013
Miss Tabata kufanyika Mei 31
Shindano la kumsaka mrembo wa Tabata,
Miss Tabata 2013, litafanyika Mei 31 katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.
Mratibu wa shindano hilo Joseph
Kapinga amesema kuwa shindano hilo litakuwa ni ya aina yake kulinganisha na
mashindano ya miaka ya nyuma kwani mwaka huu wamemejitokeza warembo wazuri
zaidi.
“Warembo wazuri wamejitokeza zaidi
kuliko mashindano ya tuliyowahi kuyafanya nyuma. Tutakuwa na burudani nyingi
kutoka nje na ndani ya nchi,” alisema mratibu huyo wa Bob Entertainment na Keen
Arts.
Warembo watakaoshiriki kwenye
shindano wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Da’ West
Park.Warembo hao ni Pendo Judica Moshi (20), Madgalena Bhoke (21), Kabula Juma
Kibogoti (20), Queen Eliakim Masha (19), Upendo Dickson Lema (22), Martha
Gewe (19), Zilpha Christopher (19), Hidaya David (22), Aneth Ndumbalo (19),
Amina Ally (18), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Kitereja
(19), Angela Fradius (19), Domina Soka (21), Rehema Kihinja (20),
Glory Jigge (18) na Sophia Claud (21).
Wengine ni Lilian Mpakani (19),
Lilian Msanchu (19), Rita Frank (20), Pasilida Mandali (21), Rafhel Mussa (19),
Jasmin Damian (18), Angelina Mkinga (19), Mercy Mwakasungu (20), Tunu Hamis
(19), Brath Chambia (23), Ray Issa (22), Shamim Abass (22) na Shan Abass
(22).
Kapinga aliwaomba warembo wenye sifa
kuendelea kujitokeza ili waweze kupata wawakilishi bora katika shindano la
Kanda ya Ilala.
"Bado milango iko wazi, mrembo
yoyote anayejiamini kwamba ana vigezo anakaribishwa. Tunataka shindano la mwaka
huu liwe na ushindani zaidi,” mratibu huyo aliongeza. Warembo 10 watachaguliwa
kushiriki mashindano ya Miss Ilala na baadaye Miss Tanzania.
Monday, April 22, 2013
DIAMOND ALIPOCHAFUA HALI YA HEWA MAISHA CLUB KWENYE KUMTAFUTA ALIEMWAGA POMBE YA MADEE , CHEKI PICHA 22 ZA SHOW ALIYOFANYA HAPA
Nilipowasili niliutana na My Big Bro Chid Benz nae akiwa amekuja kuchek show... |
Mariam & Esma khan walikuwepo kumpa support madee usiku wa Jana....pia na dada yangu halima kimwana ayupo pichani nae alikuwepo... |
Moja kwa Moja niliena backstage kuonana na madee kupanga mpango wa kumsaka aliemwaga pombe yake |
Subscribe to:
Posts (Atom)