Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Tuesday, April 23, 2013

Miss Tabata kufanyika Mei 31

Shindano la kumsaka mrembo wa Tabata, Miss Tabata 2013, litafanyika Mei 31 katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.

Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema kuwa shindano hilo litakuwa ni ya aina yake kulinganisha na mashindano ya miaka ya nyuma kwani mwaka huu wamemejitokeza warembo wazuri zaidi.

“Warembo wazuri wamejitokeza zaidi kuliko mashindano ya tuliyowahi kuyafanya nyuma. Tutakuwa na burudani nyingi kutoka nje na ndani ya nchi,” alisema mratibu huyo wa Bob Entertainment na Keen Arts.

Warembo watakaoshiriki kwenye shindano wanaendelea na mazoezi kila siku katika ukumbi wa Da’ West Park.Warembo hao ni Pendo Judica Moshi (20), Madgalena Bhoke (21), Kabula Juma Kibogoti (20), Queen Eliakim Masha (19), Upendo Dickson Lema (22), Martha Gewe (19), Zilpha Christopher (19), Hidaya David (22), Aneth Ndumbalo (19), Amina Ally (18), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Kitereja (19),  Angela Fradius (19), Domina Soka (21), Rehema Kihinja (20), Glory Jigge (18) na Sophia Claud (21).

Wengine ni Lilian Mpakani (19), Lilian Msanchu (19), Rita Frank (20), Pasilida Mandali (21), Rafhel Mussa (19), Jasmin Damian (18), Angelina Mkinga (19), Mercy Mwakasungu (20), Tunu Hamis (19), Brath Chambia (23), Ray Issa (22), Shamim Abass (22) na Shan Abass (22). 
Kapinga aliwaomba warembo wenye sifa kuendelea kujitokeza ili waweze kupata wawakilishi bora katika shindano la Kanda ya Ilala.

"Bado milango iko wazi, mrembo yoyote anayejiamini kwamba ana vigezo anakaribishwa. Tunataka shindano la mwaka huu liwe na ushindani zaidi,” mratibu huyo aliongeza. Warembo 10 watachaguliwa kushiriki mashindano ya Miss Ilala na baadaye Miss Tanzania.

Anayeshikilia taji la Miss Tabata kwa sasa Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala. Waliyojitokeza kudhamini shindano hilo ni Fredito Entertainment, CXC Africa, Brake Point na Saluti5

No comments: