STAA wa
filamu za Kibongo, Yobnesh Yusuph ‘Batuli’ amesema kama kuna mtu yeyote
anahusika na vifo vya wasanii katika ushirikina basi anajisumbua, kwake
hawafui dafu.
Batuli ameiambia Bongowood kuwa, hana uhakika kama wasanii hao vifo vyao
vinatokana na mkono wa mtu kama minong’ono iliyoenea lakini kama kuna
mambo ya nguvu za giza yanaendelea, kwake watashindwa sababu anamtegemea
Mungu.
“Sitaki kuamini sana kama hali hii inatokana na nguvu za giza lakini
kama kuna mambo ya ushirikina yanatendeka basi kwangu watashindwa kwa
uwezo wa Mwenyezi Mungu,” alisema Batuli.
No comments:
Post a Comment