Neymar Mkombozi: Mbrazil huyo anayevaa jezi namba 10 alifunga mawili.
NYOTA aliyebeba matumaini ya
Wabrazil wengi, Neymar amefunga mabao mawili usiku huu katika ushindi wa
mabao 3-1 dhidi ya Croatia kwenye mchezo wa ufunguzi wa fainali za
kombe la dunia.
Wenyeji walijifunga mapema dakika
ya 7 ya kipindi cha kwanza baada ya Marcelo kuujaza mpira nyavuni katika
harakati za kuokoa na kuzua ukimya mkubwa uwanjani kwa mashabiki wa
Brazil waliofurika kushuhudia timu yao..
Mambo almanusura yawe mabaya kwa
Brazil wakati Neymar alipomfanyia faulo mbaya kiungo wa Croatia Luka
Modric, lakini mwamuzi Yuichi Nishimura alimzawadia kadi ya njano tu.
Baadaye Neymar alifunga bao la
kusawazisha kwa shuti la mbali na aliongeza bao la pili kwa njia ya
mkwaju ya penati baada ya mwamuzi kutoa penati yenye utata kufuatia
Dehan Lovren kumfanyia madhambi Fred.
Oscar alihitimisha karamu ya mabao
kwa Wabrazil na kutoka na ushindi wa kwanza katika michuano ya mwaka
huu inayofanyika katika ardhi yao.
Mkwaju wa penati: Neymar alifunga penati yake ingawa kipa wa Croatia aligusa mpira.
Hapa chini ni viwango vya wachezaji wa timu zote na alama zimetolewa juu ya 10.
Neymar ndiye mchezaji bora wa mechi ya leo kwa kupata alama 8 akifuatiwa na Oscar mwenye alama 7.
Kikosi cha Brazil na viwango vyao: Julio
Cesar 6; Dani Alves 5.5, Thiago Silva 6, Luiz 6, Marcelo 5.5, Paulinho
6, Gustavo 7, Hulk 6 (Bernard 68), Oscar 7, Neymar 8, Fred 6.5.
Wachezaji wa akiba: Jefferson, Fernandinho, Dante, Maxwell, Henrique, Ramires, Hernanes, Willian, Jo, Maicon, Victor.
Kikosi cha Croatia na viwango vyao: Pletikosa
6, Srna 6.5, Corluka 7, Lovren 6.5, Vrsaljko 6; Modric 7, Rakitic 7,
Perisic 6.5, Kovacic 6 (Brozovic 62), Olic 6, Jelavic 6.
Wachezaji wa akiba: Zelenika, Pranjic, Vukojevic, Schildenfeld, Rebic, Sammir, Vida, Eduardo, Subasic.
Anajiangusha chini kirahisi: Fred akianguka baada ya kupewa misukosuko na Dejan Lovren na mwamuzi aliwazadia penati Brazil
Luiz Felipe Scolari akimkumbatia Neymar baada ya kufunga bao la kusawazisha.
Neymar (kushoto)akishangilia bao lake la kwanza
Guu la kushoto: Neymar akipiga shuti nje ya eneo la hatari na kuutumbukiza mpira kwenye kona
No comments:
Post a Comment