Vijana
wa Kamishina wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova
kwa kushirikiana na Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers
wamefanikiwa kulifumua danguro linalodaiwa kufuga madenti wa vyuo
mbalimbali jijini Dar.
Madenti
hao walikamatwa mwanzoni mwa wiki hii kwenye danguro hilo lililopo
ndani ya baa maarufu iliyopo maeneo ya Buguruni-Sokoni, Dar.
KERO
Awali kikosi kazi cha OFM kilipokea malalamiko kutoka kwa wazazi waishio maeneo hayo wakilalamikia ufuska wa kutisha unaofanyika kwenye danguro hilo.
Mzazi:Halooo…nazungumza na OFM?
OFM: Ndiyo…tukusaidie nini?
OFM: Tunazo nyingi lakini ukitupatia ya kwako tutaifanyia kazi ipasavyo.
Mzazi: Tunawaamini OFM mnatisha kama njaa. Sisi ni wazazi wa hapa Buguruni-Sokoni. Kuna danguro hapa kwa kweli yanayofanyika ni aibu tupu. Tunaomba mje mjionee wenyewe mfanye kazi yenu.
OFM: Nini hasa kinafanyika?
OFM: Sawa, tuachie tufanye kazi yetu.
OFM: Tunaheshimu vyanzo vyetu hatuwezi kukutaja popote kwani siyo maadili ya kazi yetu.
OFM KAZINI
Kabla ya kuwataarifu polisi juu ya kero hiyo kwa wakazi wa eneo hilo, vijana wa OFM waliingia kazini ili kujikusanyia ushahidi ambapo walipofika walishuhudia vitendo hivyo vikifanyika mchana kweupe bila kujali kama kuna serikali.
Baadhi ya makachero wa OFM walijifanya wauzaji na wengine wanunuaji ambapo walijikusanyia data za kutosha huku wakiwarekodi wahusika (madenti wanaojiuza na wanaume wanaowanunua) kwa kutumia vifaa vya kazi bila wao kushtuka.
BEI
Kuhusu bei, wapo wa bei chee kuanzia buku mbili hadi tano na wa bei mbaya ambao siyo wengi, wao wakianzia dau la elfu kumi na kuendelea.
Mmoja wa vijana hao wa OFM alifanikiwa kuingia ndani baada ya kukubaliana bei na mmoja wa wauzaji ambapo alipofika na kujionea mazingira halisi aliahirisha kwa kigezo kuwa alikuwa amepokea simu ya dharura.
USHUHUDA MBAYA
Hata hivyo, alichokishuhudia ndani, anasimulia: “Nilishuhudia watu wakiwa kwenye ‘pea’ wakijiachia kwa ngono na suala la kondom ilikuwa ni uamuzi wa mtu.
“Kondom zilizotumika zilikuwa zimezagaa kila kona yaani nilihisi mwili kunisisimka na kuwaza sana juu ya janga la Ukimwi. Kwa hali ile tumekwisha.”
TAARIFA POLISI
Ili kufanikisha zoezi la kulifumua danguro hilo, OFM iliwasiliana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi na kumweleza mchezo mzima wa uchafu unaofanyika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment