Shirika la
habari la BBC limeripoti kuwa, Takribani watu 48 wameuwawa nchini
Kenya baada ya kikundi kinachodaiwa kuwa cha wapiganaji wa kiislamu
kushambulia hoteli na kituo cha polisi katika mji wa Pwani wa nchi
hiyo.
Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa walishuhudia mapigano ya risasi yaliyodumu kwa saa kadhaa pamoja na majengo kuchomwa moto.
Kenya imekuwa ikikumbwa na mashambulizi ya kigaidi tangu mwaka 2011
wakati vikosi vyake vya kijeshi vilipoingia Somalia kwa ajili ya
kusaidia kupambana na wapiganaji wa kikundi cha al-Shabab
No comments:
Post a Comment