Pages
BRAND NEW MUSIC
metty magese
Listen & Download
http://mdundo.com/a/32626
Wednesday, June 18, 2014
Ngoma za ‘Bunyerobunyero’ zapigwa STOP na jeshi la polisi
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam
imesema itawachukulia hatua za kisheria wamiliki wa klabu za usiku
zinazokiuka maadili kwa kuruhusu klabu zao kupiga ngoma ya
‘bunyerobunyero’.
Ngoma hiyo iliibuka na kuwa maarufu hasa
jijini Dar es Salaam baada ya Polisi kupiga marufuku ngoma ya
‘kantangaze-kigodoro’ na ‘khanga moko’.
Onyo hilo lilitolewa jijini Dar es Salaam na Kamishna wa Kanda hiyo, Suleiman Kova wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Alisema ngoma hiyo imeibuka karibuni na inaenda kinyume na maadili ya Kitanzania.
Alisema ngoma hizo hazina tofauti kubwa
na vigodoro isipokuwa wahusika wa ‘bunyerobunyero wametofautisha maeneo
ya kupinga ngoma hiyo ambayo ni kwenye klabu za usiku tofauti na
vigodoro ilikuwa ikipigwa mitaani.
“Tutahakikisha kwa kushirikiana na
halmashauri za miji pamoja na polisi kuhakikisha hizi ngoma za
‘bunyerobunyero’ tunazipiga marufuku, kwasababu zinakiuka maadili,”
alisema Kova.
Alisema Polisi imetoa onyo mara nyingi
kuhusu ngoma hizo na kwamba hatua inayofuata sasa ni kuwakamata
wachezaji na wahudhuriaji wa ngoma hizo pamoja na kuwakamata wamiliki wa
klabu hizo na kuwapiga faini na kuzifungia klabu hizo.
“Onyo hili linatolewa kwasababu hizi ngoma zimeenea katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam,” alisema.
Kamanda Kova alisema ngoma hizo
zimetawaliwa na udhalilishaji wa hali ya juu jambo linalochangia
kuporomoka kwa maadili, hivyo hawatalifumbia macho.
“Uchunguzi kwasasa unafanyika na endapo
itabainika ngoma hizo kuendelea kuchezwa basi Jeshi la Polisi na
halmashauri za miji zitachukua hatua mbalimbali za kisheria ikiwa ni
pamoja na kuzifungia klabu hizo kwasababu zinakiuka taratibu za leseni,”
alisema.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment