Pages

BRAND NEW MUSIC

metty magese

metty magese

Listen & Download

http://mdundo.com/a/32626

Thursday, January 20, 2011

*WAZIRI NCHIMBI AKUTANA NA WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI LEO

Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga akimuonyesha jarida la Baraza Waziri wa Habari, vijana, utamaduni na michezo Dr. Emmanuel Nchimbi (kulia ). Wamiliki wa vyombo vya habari nchini (MOAT) na viongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) walikuwa na mazungumzo ya kujadili mambo mbalimbali kuhusiana na taaluma ya habari na waziri Dr. Nchimbi leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo. Picha na Anna Nkinda - Maelezo
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (Maelezo) Raphael Hokororo, akifafanua jambo kuhusu sera ya habari wakati wa mazungumzo kati ya wamiliki wa vyombo vya habari nchini (MOAT), na viongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Waziri wa Habari, vijana, utamaduni na michezo Dr. Emmanuel Nchimbi katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo. Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Kajubi Mukajanga. Mwenyekiti wa wamiliki wa vyombo vya habari nchini Reginald Mengi (kulia) akizungumza jambo wakati wa mkutano huo leo. Kushoto ni Waziri wa habari, vijana, utamaduni na michezo. Anayemsikiliza ni Waziri wa Habari, vijana, utamaduni na michezo Dr. Emmanuel Nchimbi .Waziri wa Habari, vijana, utamaduni na michezo Dr. Emmanuel Nchimbi (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wamiliki wa vyombo vya habari nchini (MOAT) na viongozi wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) mara baada ya kumalizika kwa mkutano wao ulioganyika leo katika ukumbi wa mikutano wa wizara hiyo.


WANARIADHA WAPATA MSAADA WA VIFAA VYA MICHEZO

                                     Mwanariadha MASUMBUKO akikabidhiwa vifaa vya michezo
                                                          SARAH akikabidhiwa vifaa vya michezo na NCHIMBI
wanariadha wataowakilisha nchi
Hapo jana Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na Michezo amekipazia sauti chama cha riadha Tanzania akiwaomba wadhamini binafsi kujitokeza kuusaidia mchezo huo.

Waziri NCHIMBI ametuma maombi haya kwa wadauwakati akikabidhi vifaa vya michezo kwa wanariadha wawili wa Tanzania watakaoshiriki kwenye mashindano ya riadha ya kimataifa yatakayofanyika huko BAMAKO MALI baadae mwezi huu.

JEASHI LA CONGO 'LILIONGOZA UBAKAJI'

Kamanda wa jeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameshutumiwa kwa kuongoza ubakaji wa wanawake takriban 50 uliofanyika hivi karibuni.Kumekuwa na ripoti nyingi za ubakaji huko Congo lakini tukio hili linaaminiwa kuwa la kwanza kwa idadi kubwa ya wanawake kubakwa likihusishwa jeshi. Mmoja wa waliobakwa, pamoja na vyanzo vilivyonukuliwa katika ripoti ya umoja wa mataifa, wote wanamshutumu Lt Col Kibibi Mutware kwa kuhusika na ubakaji huo uliofanyika mwaka mpya mjini Fizi.

Dr Faise Chacha, mkuu wa hospitali ya Fizi ameeleza, " Askari mmoja aliuawa hapa karibu kabisa na hospitali hii." "Hiyo ilisababisha wasiwasi na wagonjwa wetu wote wakakimbia. Tulirudi siku ya pili asubuhi na tukaanza kuwapokea watu waliokuwa wamepigwa kisu na wengine- wanawake- waliobakwa." Dr huyo na shirika la kitabibu la kutoa msaada Medecins Sans Frontieres wamewatibu waathirika 51 waliobakwa mpaka sasa.

Kama ilivyo kwa matukio ya awali huko Congo, wengi wanatarajiwa kuficha yaliyowasibu kuepuka kuachwa na waume na familia zao. Wawili miongoni mwa wanawake hao walikubali kuzungumza na BBC ilimradi tu wasitajwe majina yao.

Mmoja aliiambia BBC, " Nilibakwa mbele ya watoto wangu wanne." "Ninaona aibu, ninaona aibu sana. Nikikutana na watu wawili au watatu ambao wanajadili jambo, naanza kuhisi tu kuwa wananizungumzia mimi, hata kama si kuhusu mie."

Mwanamke huyo mwengine alifanikiwa kumtambua aliyembaka. "Ilikuwa jioni na walionibaka walikuwa wanajeshi," alisema kwa sauti ndogo, mwili wake ukiwa umefunikwa na khanga yenye rangi za kuvutia. nakuongeza kwa kusema " Walikuwa wanne- Kibibi na walinzi wake. Wameiba vitu vyetu vyote pamoja na pesa."


TAIFA STARS YALAMBA MILIONI 75

WAANDAAJI wa michuano ya soka kwa Nchi za Bonde la Mto Nile wameipa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' sh.milioni 75, ingawa ilivurunda.

Taifa Stars ilishika nafasi ya sita kati ya timu saba zilizoshiriki mashindano hayo ya kwanza ambayo yameandaliwa na Misri,huku Burundi ikiwa ndiyo ya mwisho na Sudani imeshika nafasi ya tano, baada ya Jumapili kuifunga Taifa Stars mabao 2-0 katikamechi ya kuwania nafasi ya tano.Lakini juzi Taifa Stars, Sudani na Burundi timu vibonde katika mashindano hayo zilitangazwa kila moja kupewa dola za Marekani50,000 sawa na sh. milioni 75 za Tanzania. Mashindano yaliandaliwa na Chama cha Soka cha Misri (EFA).

Fedha hizo ziliztangazwa baada ya mchezo wa fainali ya michuano hiyo Uwanja wa Jeshi mjini hapa ambapo Misri iliibuka naushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Uganda na kuibuka bingwa.

Kwa kutwaa ubingwa huo ambao unaifanya Misri kuwa bingwa wa kwanza ilizawadiwa dola 150,000 za Marekani sawa na sh. milioni225 za Tanzania, wakati Uganda iliyoshika nafasi ya pili ilizawadiwa dola za Marekani 120,000 sawa na sh.milioni 180 zaTanzania.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ambayo juzi iliifunga Kenya baop 1-0 ma kushika nafasi ya tatu, yenyewe ililamba dolaza Marekani 100,000 sawa na sh. milioni 150 za Tanzania, huku Kenya yenyewe ikitia kibindoni dola 60,000 sawa na sh.milioni90 za Tanzania.

Dola moja ya Marekani kwa sasa ni kati ya sh.1460 hadi 1500 hivyo kuifanya angalau Taifa Stars nayo kupoza machungu ya kukosazawadi kubwa za mshindi wa kwanza hadi wa tatu.

Taifa Stars ambayo haikushinda mechi katika mechi ilitarajiwa kuondoka jana usiku na kufika Dar es Salaam leo alfajiri ikiwa,ikiwa imefungwa mechi mbili na kutoka sare mbili Ilifungwa na Misri mabao 5-1, ilifungwa na Sudani mabao 2-0 na ilitoka sare ya bao 1-1 na Uganda na sare kama hiyo na timuiliyoshika nafasi ya mwisho Burundi, ambayo ilipata pointi moja tu ya Stars.

Wakati huohuo, kipa Kidiaba wa DRC alitangazwa kuwa Kipa Bora wa Mashindano, huku mshambuliaji Said Khamdi wa Misri ambayemechi ya fainali alifunga mabao mawili alitangazwa kuwa Mfungaji Bora baada ya kufunga mabao sita na Ahned Said Faraj pia waMisri aliibuka Mchez
aji Bora.

Pongezi wakati wa uzinduzi wa Kilimanjaro Tanzamia Music Award's 2011 usiku huu katika hoteli ya Double Tree jijini Dar.
Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja akizungumza katika uzinduzi wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Award's 2011 uliofanyika usiku huu katika hotel ya Double Tree Hilton,Masaki jijini Dar.
Meneja wa bia ya Kilimanjaro,George Kavishe akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika usiku huu katika hotel ya Double Tree Hilton,Masaki jijini Dar.
Katibu Mkuu wa BASATA,Gonche Materego akizungumza katika uzinduzi huo uliofanyika usiku huu katika hotel ya Double Tree Hilton,Masaki jijini Dar.

Muwakilishi wa Wasanii wa Music nchini,Luiza Mbuttu akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake wote.
Msanii wa muziki wa Bongo Freva,Marlow akifanya vitu vyake katika uzinduzi huo.
Msanii wa Muziki wa kizazi kipya,Mataluma akikamua usiku huu katika uzinduzi wa tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music Award's 2011 uliofanyika usiku huu katika hotel ya Double Tree Hilton,Masaki jijini Dar.
MC wa shughuli hiyo,Gardiner Habash akiwajibika ipasavyo katika uzinduzi huo.Ankal akiwa na Wadau wa TBL,Shoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja na kulia ni Meneja wa bia ya Kilimanjaro,George Kavishe.
Mbunifu wa Mavazi na Mwanamitindo mkongwe hapa nchini,Khadija Mwanamboka akijadiliana jambo na Mrembo Jokate Mwegelo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kilimanjaro Tanzania Music Award's 2011 uliofanyika usiku huu katika hotel ya Double Tree Hilton,Masaki jijini Dar.
Wakali wa Bongo Flava.
Miamba ya Kaskazini ikiwakilisha kama kawa.
Amini na Linah wakiwa katika mazungumzo ya hapa na pale.
toka kulia ni Giver Meena,Martin na Mdau.
Wadau wa TBL wakiwakilisha katika uzinduzi huo.
Ma DJ's wa Ukweli kutoka katika familia moja,toka shoto ni Dj Bon Lov,Dj Mackay na Dj Venture.
Mkurugenzi wa Masoko wa TBL,David Minja akiwa na Mdau Ben Kisaka pamoja na Miss Tanzania 2010,Genevive Emmanuel katika hafla hiyo ya uzinduzi wa Kilimanjaro Tanzania Music Award's 2011 uliofanyika usiku huu katika hotel ya Double Tree Hilton,Masaki jijini Dar.
Wadau,toka shoto ni Hud,Sylvia Sharry,Martin pamoja na Jamillah.
Msanii wa Bongo Freva,Mwasiti (shoto) akila na Richard,Hamis B 12 na Linda.
Aunt Ezekiel Wadau wenzake katika nyanja ya Filamu.
Wasanii wa Bongo Freva wakiimba wimbo wa pamoja unaohusu Kilimanjaro Tanzania Music Award's usiku huu.
Mamaa wa 8020 Fashions,Shamim Mwasha akiwaonyesha taswirazz kwa warembo mara baada ya kuipata kupitia kamera yake.
Mtu mzima Bon Lov na Banana Zorro pamoja na C Pwaa.
Wadau.
Benjamin wa Mambo Jambo (shoto) akiwa na washkaji wengine wakifuatilia shughuli nzima ya uzinduzi huo usiku huu.
Temba na Chegge wakishow love na mdada wa Double Tree Hilton usiku huu.
toka shoto ni Ahmad Michuzi,Abraham Mossi na Mdau.
Wadau wa TBL wakibadilishana mawazo wakati wa hafla hiyo usiku huu.

Wadau wa Taarab pia walikuwepo.
Wafanyakazi wa TBL.
Wadau

Wednesday, January 19, 2011

JESHI LA POLISI LANASA VIPUSA VYA FARU JIJINI MWANZA


Polisi mkoani Mwanza, imewakamata watu wawili akiwamo afisa wa wanyama pori, Allchraus Jacob (31),na Kasika John (44) ambaye ni mkuluma wa wilayani Bunda, wakijaribu kuuza pembe za kifaru maarufu kwa jina la George (12) akifahamika kama faru wa Rais Jakaya Kikwete, aliyeuawa na majangili, Desemba mwaka jana. Jeshi hilo limekamata Vipusa vya Faru vikitembezwa sokoni kutafuta Mteja, Inasemekana kuwa pembe hizi za faru (Vipusa) hutumika kutengenezea dawa ya kuongeza nguvu za Kiume huko katika nchi za Falme za Kiarabu, Japan, Korea na hata china ambako vinasoko kubwa sana.

#####WAKATI HUO HUO jeshi la polisi mkoani mwanza lanawashikilia watu wanne, wawili kati yao wakiwa na bunduki aina ya SMG na risasi 64 ambazo zilikuwa zimefichwa ndani ya begi la nguo zikisafirishwa kwenda wilayani Geita..Kaimu wa polisi amesema kuwa watuhumiwa ambao walikamatwa na begi hilo la silaha walijitambulisha kama mke na mume na kwamba walikuwa wakielekea katika kijiji cha Bukondo wilayani Geita.

Ndani ya begi hilo kulikuwa na viatu vya kike, panga moja na shoka ambavyo vilikuwa vimefungwa katika mfuko wa sandarusi pamoja na vikaratasi vidogovidogo vilivyokuwa vimefungwa dawa mbalimbali za mitishamba ambavyo walidai kuwa ni hirizi za dawa za kusaidia wakati wa matukio ya ujambazi.

Baada ya kuwakamata watu hao waliweza kuwataja wenzao ambao walikuwa bado hawajaondoka Mwanza kuungana nao katika shughuli zao za uharamia, ambao nao waliweza kukamatwa eneo la Nyegezi wakiwa na mkakati wa safari kuelekea ambako walipanga kufanya uhalifu mwingine..


 KIINGLIO CHA SIMBA NA ATLETICO BWERERE...!!


Rais wa Kampuni ya RPB, Rahma Al Kharoous, akizungumza na waandihi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki katika ya Yanga na Atletico ya Brazir uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa leo jioni.

KUTOKANA na muitikio mdogo wa mashabiki wa soka waliojitokeza kushuhudia mchezo wakirafiki baina ya Yanga ya Dar es Salaam na Atletico Paranaense ya Brazir kwenye Uwanja wa Taifa leom, Rais wa Kampuni ya RPB Oil, Rahma Al Kharoous, amesema kuwa mchezo wa keshokutwa kati ya Simba na timu hiyo kiingilio itakuwa ni bure.
Akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Rahma, ambaye ndiye mratibu wa michezo hiyo ya kirafiki, alisema kuwa ameamua kufanya kiingilio kuwa bure ili mashabiki wengi waweze kujitokeza kushuhudia mchezo huo na kuishangilia timu ya Simba ili kuwapa morari waweze kushinda.

Aidha alisema kuwa iwapo Simba itaweza kuibuka na ushindi basi ataigharamia timu hiyo ya Simba kuisafirisha hadi nchini Brazir kwa ajili ya mchezo wa marudiano na kuwataka mashabiki wengi kujitokeza kushuhudia mchezo huo.

Ndugu mtazamaji kama unavoona mechi ya jana kwenye picha watu walikuwa kidogo sana kulinganisha na ukubwa wa mechi hiyo
  JE UTAMADUNI HUU HAUMZALILISHI MTU KINSIA?...WADAU....!!!
 Makirikiri walipoanza show yao Usiku wa kuamkia Januari 15, 2010 katika kumbi wa Wenge Garden Ukonga Mombasa Dar es Salaam.
 Staili hizi ziliwakosha sana wapenzi wa ngoma hizo za asili kutoka nchini Boswana.


2011 TANZANIA WOMEN OF ARCHIEVEMENT AWARDS

Frontline Porter Novelli, a local PR and communications firm, today launched the Tanzania Women of Achievement Awards that is due to take place on the international women’s day (8th of March 2011).

These annual awards were first launched in 2009 in honor of women across the country who have been at the forefront of achieving political, economical and social equality in their communities.

TWAA seek to recognize women, currently working in the geographical boundaries of Tanzania, paying tribute to the most exceptional and achieving women in the country who have not only achieved success in their own respective fields but who through their work and initiatives have made a significant difference in their community and society as a whole.

“The Awards provide a wonderful opportunity to recognize and applaud women who are helping to reshape Tanzania for the better. For many of the women this will be the first time that their achievement has received public accolade. The nominated women are awarded cash prize as well as a trophy and certificate signed by the current patron who is the UWT chairlady Mama Sophia Simba at a dinner gala attended by the corporate, government, NGO’s and diplomatic community.” Said Irene Kiwia, Managing Director of Frontline Porter Novelli. “To add more value to the awards, this year TWAA will incorporate a mentorship program where young emerging women leaders from different villages across the country will be identified and paired with women executives in politics and business for a 3 weeks mentorship program that aims at combining leadership training, networking and professional development to provide the mentees with the tools that they need to succeed as well as teach them a “pay it forward’ model of leadership that promotes the mentees efforts to promote positive changes in their communities”.

The Categories for this year’s awards are Arts and Culture, Business Entrepreneur, Information and Communication, Sports, Professional, Education, Health, Social Welfare, Science and Technology, Public Sector, Young Achiever, Agriculture, Lifetime Achievement and the overall Woman of the Year.

“We urge organizations, associations, women and men across Tanzania to nominate women in these categories and play a role in gender empowerment. There are thousands of deserving women out there who through their work have had significant impacts in their communities. We want to sing the praises of these unsung heroes and inspire millions of other Tanzania women to take charge and make a change” said Mrs. Sadaka Gandi, the TWAA committee chairperson, a Social Counselor and Psychologist. “We received a lot of nominations in the first TWAA but expect much more this time.”


The TWAA committee comprises of Mrs. Mary Rusimbi – Activist and Founder of Tanzania Gender Networking Program, Dr. Ramadhani Dau – Director General National Social security Fund,  Joaquine De Mello - Commissioner for the Commission of Human Rights and Good Governance, Dr. Marcelina Chijoriga – Dean University of Dar es Salaam Business School,  Mrs Jacqueline Lenhardt – Spouse of the US Embassy Ambassador, Innocent Mungy- Communication Director Tanzania Communication Regulatory Authority, Sadaka Gandi – Counselor Psychologist and Social worker, Irene Kiwia – Founder and Managing Director Frontline Porter Novelli and is sponsored by Serengeti Breweries through its Baileys brand, Delloite, NBC, Home Shopping Center, TCRA, Songas, The American People, DTP and the UN Development Partners Gender 


Group.jAKAYA AKITOA SALAMU ZA RAMBIRAMBI NA HESHIMA YA MWISHO KWA KIFO CHAMH.JAJI MAPIGANO