MWANAUME
aliyefahamika kwa jina la baba Salome, mkazi wa Tandika jijini Dar es
Salaam, hivi karibuni alimdhalilisha mkewe (mama Salome) baada ya
kufumaniwa gesti akiwa na mwanaume mwenzake ambapo madai yalisema,
walikuwa katika hatua za mwisho za kuingiliana kimwili...
Aibu hiyo ya
mwaka ambayo ilionekana pia kama kituko ilijiri Mei 3, mwaka huu ndani
ya gesti moja maarufu iliyopo Devi’s Corner –Tandika, jijini Dar es
Salaam.
Awali
ilidaiwa kuwa, mwanaume huyo na baba Salome mwenye mke na watoto wawili
wanaomtegemea kwa kila kitu, walionekana wakiingia kwenye gesti moja
ambayo pia ipo maeneo hayo hali iliyozua maswali kwa watu waliokuwa
wakiwafahamu.
“Unajua
tatizo lilianzia wapi? Baba Salome na yule mwanaume mwenzake
walionekana wakiingia gesti moja kisha wakatoka, wakaingia nyingine pia
wakatoka, ndipo watu wanaowafahamu wakajiuliza kulikoni wawili hao
kutembelea gesti siku hiyo, wakawafuatilia,” alisema mnyetishaji mmoja.
Akaendelea:
Lakini watu waliwafahamu kwa namna mbili tofauti, baba Salome ni
mtulivu, mwadilifu, mwenzake watu wanasema ana ‘katabia’ ka kutaka kuwa
faragha na wanaume wenzake bila kujulikana nini anakitaka katika usiri
huo.
Madai
zaidi yakawekwa wazi kwamba, baadhi ya watu walikwenda kwenye gesti
walizokwenda wawili hao na kuulizia nini walikuwa wanakitaka, ndipo siri
ikawekwa wazi kwamba wanatafuta chumba cha kupumzika kwa siku hiyo
lakini kwa sheria za Jiji la Dar es Salaam (kama siyo za nchi nzima),
wanaume wawili hawaruhusiwi kulala chumba kimoja.
Chanzo
kikasema: Wambeya wakawaona wakiingia kwenye gesti ya tukio, wakapewa
chumba. Ndipo wakakimbia nyumbani kwa baba Salome na kumtonya mkewe,
mama Salome kwamba mumewe ameingia gesti.
Kichekesho
zaidi kinaangushwa kwamba, baada ya kuambiwa mumewe amezama gesti, mama
Salome ambaye ndiyo kwanza alikuwa amefika kutoka kwenye mikopo ya
Finca, alitoka mbio huku akisema anakwenda kumtoa sikio la kulia Kidawa
akiamini mumewe ameingia gesti na mwanamke huyo. “Watu
walimwambia mumewe hakuingia gesti na Kidawa bali mwanaume mwenzake.
Kwanza mama Salome aliomba asitaniwe juu ya hilo, lakini akasisitiziwa,”
alisema mtoa habari huyo.
Akizungumza
kwa jazba na waandishi wetu nje ya gesti hiyo, mama Salome alisema
kwamba alipata taarifa siku nyingi mumewe ana ukaribu na mwanaume huyo
ambaye mitaani watu wanasema anajihusisha na vitendo vya ushoga.
“Nilipozipata
taarifa hizi sikuziamini, nilidhani ni Kidawa ndiyo kaingia gesti na
mume wangu, maana Kidawa ndiye mbaya wangu,” alisema mwanamke huyo kisha
akazama ndani ya gesti akiwa na polisi ambao haikujulikana walikotokea.
Huku
mumewe na mwanaume mwenzake wakiwa hawana hili wala lile kule chumbani,
mlango ulisukumwa na kufunguka ambapo mwanamke huyo aliwakuta wawili
hao wakiwa wameshavua baadhi ya nguo.
Wote walishtuka kuona
wameingiliwa!
“Yaani
roho inauma sana, sijui ni kitu gani umekosa kwangu mpaka unakuja kwa
mwanaume mwenzako jamani baba Salome,” alisema huku akilia mama Salome.
Baada
ya kugundua wamenaswa, mwanamke aliyekuwa na baba Salome aliangua kilio
huku akiomba kusamehewa kwa vile yeye ni mume wa mtu, lakini kilio
chake hakikusikika kwa polisi ambapo waliwafunga pingu na kuwataka
kuelekea katika kituo cha polisi.
Wakati
wakitoa maelezo kwenye kituo cha polisi, mwanaume aliyekuwa na baba
Salome alijitambulisha kwa jina la Julius Mwita, mkazi wa Devi’s Corner
ana mke na watoto wawili na aliwaomba sana waandishi wamhifadhi kwani
wakwe zake wakimuona ‘itakula kwake’.