Kwa
mujibu wa mwakilishi wa mwanamuziki huyo, Jennifer Lopez hatashiriki
sherehe za mwaka huu za ufunguzi wa kombe la dunia ambapo hajatoa sababu
ya kufikia uamuzi huo.
Lopez
aliungana na rapa Pitbull pamoja na nyota wa nchini Brazil Claudia
Leitte kwa ajili ya kurekodi wimbo maalum wa kombe la dunia kwa mwaka
huu uliopewa jina la “We Are One (Ola Ola).”
Wanamuziki
hao watatu kwa pamoja walitakiwa kuimba wimbo huo katika sherehe za
ufunguzi katika mechi ya kwanza lakini Jlo amesitisha na kusema
hatokuwepo tena.
No comments:
Post a Comment